Kampuni yatangaza viwanja zaidi ya 100 kwa Vijana na Wanawake
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kampeni ya Shoham Property Developers imeanza kampeni maalum ya kuuza viwanja vilivyopimwa hususani kwa vijana na akina mama lengo likiwa ni kuwawezesha kumiliki viwanja visivyo na migogoro kwa gharama nafuu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Mkurugenzi wa kampuni Shoham, Mengi Lubambo alisema gharama za viwanja hivyo inaanzia shilingi milioni mbili ambapo viwanja vinapatikana nje kidogo ya jiji la Mwanza.
“Ukinunua kiwanja Shoham utaondokana na migogoro ya ardhi kwani tunauza viwanja vilivyopimwa vikiwa na hati tofauti na wengine ambao wamekuwa wakiuza viwanja ambavyo havijapimwa kwa mtu zaidi ya mmoja” alisema Lubambo.
Naye Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Amina Salim alisema kampeni hiyo imewalenga vijana zaidi kwani wao ndio wajenzi wa Taifa hivyo ni vyema wakamiliki ardhi zisizo na migogoro kwa ajili ya uwekezaji badala ya kutegemea mali za urithi.
“Viwanja vyetu pia vina miundombinu muhimu ikiwemo maji, umeme na barabara ambapo tumeamua kuvitoa kama zawadi kwa vijana na akina mama kwa bei nafuu ya shilingi elfu nane kwa ‘square meter’ moja huku malipo yakifanyika kwa awamu” alisema Salim.
Kwa Mahitaji ya Kiwanja/ Viwanja 0786 38 97 00
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari zaidi hapa
No comments: