LIVE STREAM ADS

Header Ads

SUZA wakabiliana na wimbi la tatu la Covid 19

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Dickson Billikwija, Dar es Salaam
Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (SUZA) kinaendelea kuchukua tahadhari ili kupambana na wimbi la tatu la maambukizi ya janga la virusi vya Corona (COVID-19).

Akizungumza wakati wa Maonesho ya Vyuo Vikuu ambayo yanasimamiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Mkuu wa Kitengo Cha Udahili Chuoni hapo, Ali Shauri Jecha amesema wanazingatia masharti ya kiafya yanayotolewa na Serikali pamoja na wataalamu wa afya ikiwemo kuvaa barakoa, unawaji mikono kwa sabuni na maji tiririka.

Aliongeza kuwa hata kwenye Maonesho hayo kuna barakoa ambazo zimetengenezwa na chuo pamoja na vitakasa mikono (Sanitizer) ikiwa ni sehemu ya kujikinga na maambukizi ya janga hilo la Corona.

Naye Khadija Mahumba ambaye ni Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano na Masoko aliwakaribisha watu wote kwenye Maonesho hayo akisisitiza kufika katika banda la chuo hicho ili kujifunza fursa mbalimbali zilizopo.

No comments:

Powered by Blogger.