LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyakazi TANESCO wahimizwa kufanya mazoezi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Ziwa wametakiwa kujiwekea utamaduni wa kufanya mazoezi kila mwisho wa juma ili kujiimarisha kiafya na kutimiza vyema majukumu yao.

Rai hiyo ilitolewa na Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato wakati akifungua Bonanza la Michezo TANESCO Kanda ya Ziwa lililofanyika katika uwanja wa Nyamagana likijumuisha wafanyakazi kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Geita na Kagera.

"Ni vizuri Ijumaa au Jumamosi kila Mkoa ujiwekee utaratibu wa kufanya mazoezi na hii ni kwa ajili ya afya zetu na kuimarisha mahusiano kazini. Tukifanya hivyo hata huo ugonjwa tunauogopa (Corona) tutaufukuza kwa njia ya mazoezi pamoja na maombi" alisisitiza Mhandisi Byabyato.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi, Amos Mtae aliomba bonanza hilo kufanyika kila baada ya miezi mitatu kwa kuzunguka katika mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa ambapo ombi hilo lilikubaliwa na Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato.

Bonanza la Michezo TANESCO Kanda ya Ziwa lilitamatika kwa timu ya soka ya Tanesco Mkoa Kagera kuibuka bingwa baada ya kuichabanga goli 2-0 timu ya Tanesco Mkoa Mwanza ambapo kwa mpira wa pete timu ya wanawake Tanesco Mkoa Mwanza iliibuka bingwa baada ya kuichakaza timu ya Tanesco Kanda ya Ziwa kwa magoli 45 kwa 20. 

Bonanza hilo pia lilijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba, kukimbia na magunia, kufukuza kuku na mazoezi ya viungo lengo likiwa ni kuimarisha afya pamoja na mahusiano kazini miongoni mwa watumishi wa TANESCO.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato akifungua Tamasha hilo.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato (wa watu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na manahodha na waamuzi wa soka kwenye bonanza hilo.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato akikagua kikosi cha timu ya mpira wa Pete TANESCO Kanda ya Ziwa.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato akizungumza na wachezaji wa mpira wa pete TANECO Mkoa Mwanza na Kanda.
Kikosi cha timu ya soka ya TANESCO Mkoa Kagera.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga baada ya kuibuka mabinwa kwenye bonanza hilo.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya soka ya TANESCO Mkoa Kagera baada ya kuibuka bingwa kwenye bonanza hilo.
Mhandisi wa Miradi TANESCO Mkoa Mwanza, Godfrey Vomo akitoa salamu za Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Felix Olang wakati wa kuhitimisha tamasha hilo.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato akitoa neno la kuhitimisha bonanza hilo.
Baada ya bonanza hilo, wafanyakazi wa TANESCO Kanda ya Ziwa walijumuika kwenye mchapalo wa jioni kuwaaga wafanyakazi wenzao waliostaafu, waliohamia vituo vingine vya kazi na kuwakaribisha wapya.
Burudani ikiendelea...
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato akitoa neno la ufunguzi kwenye mchapalo huo.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato akitoa zawadi kwa wafanyakazi wa TANESCO Mkoa na Kanda ambao wamestaafu.
Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Felix Olang' (kulia) akipokea kikombe kutoka kwa timu ya TANESCO Mkoa Mwanza baada ya kuibuka bingwa kwenye Bonanza la TANESCO Kanda ya Ziwa.
Wasaa wa maakuli...
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.