Mitaa 38 wilayani Ilemela kuunganishiwa umeme
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria hafla ya uwashaji umeme katika Zahanati ya Nyamwilolewa Wilaya Ilemela mkoani Mwanza ambayo ilijengwa takribani miaka 50 iliyopita lakini ilikuwa haijafikiwa na nishati hiyo.
Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt. Angeline Mabula, Katibu wa CCM Wilaya Ilemela, Diwani wa Kata ya Shibula Swila Dede, Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza Emil Kasagala na Mkuu wa Wilaya Ilemela Hassan Masala.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye kinasa sauti) akizungumza baada ya kuwasha umeme katika Zahanati ya Nyamwilolewa wilayani Ilemela.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amemtaka mkandarasi kampuni ya NAMIS kuhakikisha ndani ya miezi 12 awe amesambaza umeme katika Mitaa yote 38 ambayo haijafikiwa na nishati hiyo katika Wilaya Ilemela mkoani Mwanza.
Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo wakati akiwasha umeme katika Zahanati ya Nyamwilolelwa Kata ya Shibula wilayani Ilemela ambayo kwa takribani miaka 50 tangu ianzishwe haikuwa na nishati hiyo huku akionya suala la wananchi kuunganishiwa umeme kwa gharama za juu tofauti na elfu 27 kama ilivyoelekezwa na Serikali.
“Nimesema umeme ni elfu 27, na kwa vile hapa ni mjini, uwe una hela nyingi au hauna hela nyingi umeme ni elfu 27 tu. Nimetoa maelekezo kwa wakandarasi, nataka mitaa yote ienee umeme, wananchi mtalipia hapa hapa na si kwenda ofisi ya Tanesco Wilaya” alisisitiza Dkt. Kalemani.
Katika hatua nyingine Dkt. Kalemani alizindua mradi wa kusambaza umeme awamu ya pili katika maeneo ya pembezoni mwa miji na majiji (Peri Urban) katika Wilaya Ilemela ambapo takribani shilingi bilioni 10 zinatarajiwa kutumika kufikisha umeme katika mitaa 59 ya miji na majiji mkoani Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: