LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Jafo asitisha shughuli za uchenjuaji dhahabu wilayani Rorya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira, Selemani Jafo (kushoto) akimsikiliza Mwita Ngusui (kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakihenene wilayani Rorya wakati akiwasilisha malalamiko yake juu ya kukithiri kwa uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za uchenjuaji wa dhahabu katika mgodi wa Double F ulipo katika Kijiji cha Nyakisya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo (kushoto) akitoa maelekezo ya Serikali kwa Is-haka Juma ambaye ni Msimamizi wa mgodi wa Double F kuhusu takwa la kisheria la kufanya ukaguzi wa mazingira katika eneo la uchenjuaji wa dhahabu. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka na Mbunge wa Jimbo la Rorya, Jafari Chege.

Mwonekano wa eneo linalolalamikiwa na wakazi wa Kijiji cha Nyakisya wilayani Rorya kwa uchafuzi wa mazingira. Waziri Jafo amesitisha shughuli za uchenjuaji katika eneo hilo kupisha uchunguzi wa kimaabara.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo amesitisha shughuli za uchenjuaji wa dhahabu katika mtambo wa double F katika Kijiji cha Nyakisya Wilaya Rorya mkoani Mara kutokana na uchafuzi wa mazingira.

Jafo ametoa maagizo hayo kufuatilia malalamiko ya wananchi kuhusu athari za kiafya na kimazingira zinazo sadikika zinazotokana na kemikali ya 'cyanide' inayotumika katika shughuli za uchenjuaji wa dhahabu na kutiririka katika chanzo cha maji cha Senye.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa maeneo hayo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakihenene Mwita Ngusui amesema wakazi wengi na vitongoji vya maeneo ya jirani kwa kiasi kikubwa wameathirika na kemikali hiyo.

Kufuatia hatua hiyo, Jafo amesema kikosi kazi kinachoundwa na Taasisi za Serikali ikiwa ni pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Mkemia Mkuu na Bodi ya Bonde la Ziwa Victoria kwa pamoja kuchunguza na kutoa taarifa za kitaalamu kuhusu maji hayo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Jafo amesema Ofisi yake haitamvumilia mwekezaji yeyote anaeharibu mazingira na kuathiri afya za watu. Katika hatua nyingine Waziri Jafo amebaini ukikwaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kwa mgodi huo wa double F kwa kuanza shughuli ya uchenjuaji bila kufanya Tathmini ya Athari kwa mazingira.

Amemwelekeza Msimamizi wa Mtambo huo wa Double F, Is-haka Juma kuwalisiliana na Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mapema iwezekanavyo ili ukaguzi wa mazingira uweze kufanyika.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa maeneo hayo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakihenene Mwita Ngusui amesema kuwa wakazi wengine wa maeneo hayo na vitongoji vya jirani kwa kiasi kikubwa wameathirika na kemikali hiyo.

Nae Mbunge wa Jimbo la Rorya, Jafari Chege ameishukuru Serikali kwa kusikia kilio cha wananchi wa Rorya na kuchukua hatua za ufuatiliaji.

No comments:

Powered by Blogger.