LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bilionea wa Hotel za Gold Crest kuzikwa jijini Arusha

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amesaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa mmiliki wa Hoteli za Gold Crest zilizopo Arusha na Mwanza, bilionea Mathias Manga.

Mhandisi Gabriel amesema  marehemu Manga atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika jamii kutokana na shughuli zake za kibiashara zilizosaidia kutoa ajira hususani kwa vijana.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akiwasili katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza kusaini kitabu cha maombolezo cha Bilionea Mathias Manga.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia msiba wa aliyekuwa mmiliki wa Hotel za Gold Crest zilizopo Arusha na Mwanza, marehemu Mathias Manga.
Taratibu za mazishi ya bilionea Mathias Manga zinatarajiwa kufanyika baada ya mwili kuwasili kutoka Afrika Kusini Alhamisi Agosti 19, 2021 ambapo atazikwa mkoani Arusha.

No comments:

Powered by Blogger.