LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanza wazindua zoezi la Chanjo ya UVIKO 19

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Roberth Gabriel amezindua rasimi zoezi la utoaji chanjo ya Uviko 19 lililofanyika katika viwanja vya Hospital ya Mkoa wa Mwanza ya Sekoutoure jijini Mwanza.

Akizungumza Agosti 03, 2021 wakati wa uzinduzi huo, Mhandisi Gabriel amewataka wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo na kuacha kusikiliza habari za upotofu zinazozungumzwa hasa mitandaoni kuhusiana na chanjo hiyo. 
Mhandisi Gabriel amesema awamu hii ya kwanza ya utoaji chanjo hiyo itahusisha makundi maalumu wakiwemo watoa huduma za afya, watu wenye umri wa kuanzia miaka 50 na wale wenye magonjwa sugu.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Thomasi Rutachunzibwa amesema Mkoa wa Mwanza umepokea chanjo dozi 2,000 ambazo tayari zimesambazwa katika Halmashauri zote nane mkoani humo.

Dkt. Rutachunzibwa amesema vituo 27 vimetengwa kwa ajili kutoa huduma ya uchanjaji wa chanjo hiyo ambapo kila Halmashauri itakuwa na vituo vitatu hadi vitano kulingana na uhitaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amesema wamepokea taarifa za kufika kwa chanjo kwa furaha kubwa na kuahidi kuendelea kuwaelimisha wananchi ili waweze kufika katika vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kupatiwa chanjo.

Amesema kwa Wilaya ya Nyamagana kuna vituo vitatu vimetengwa katika maeneo ya Sekoutoure, Butimba na Kangaye.
Tazama BMG TV hapa chini
Na Tonny Alphonce & Cyprian Magupa, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.