LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watoto kutopatiwa Chanjo ya UVIKO 19

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Imeelezwa kuwa watoto wadogo hawapo katika makundi yaliyopewa kipaumbele katika kupatiwa chanjo ya kupambana na wimbi la tatu la Corona ambayo imeanza kutolewa nchini mara baada ya kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Dokta Tumaini Haonga ambaye ni Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma katika Magonjwa ya Mripuko kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wakati akijibu maswali ya wadau katika kikao kazi cha timu ya uhamasishaji wa afua za afya mkoa wa Mwanza.

Dkt Ahonga alisema makundi ambayo yamepewa kipaumbele ni makundi ambayo yapo hatarini zaidi kupatwa na ugonjwa wa Corona ili kuyakinga makundi hayo kwanza wakati jitihada za kupata chanjo za kuwachanja watanzania wote zikiendelea.
Aliyataja makundi ambayo yamepewa kipaumbele katika awamu hii ya kwanza ni watoa Huduma za Afya,Wenye magonjwa ya muda mrefu kama Kisukari,Moyo na shinikizo la damu.

Alisema utafiti uliofanyika umeonyesha watoto wenye umri wa kuanzia mwaka 0 hadi 15 hawapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Corona na badala yake watu wenye umri wa miaka 45 na kuendelea wameonekana wapo hatarini zaidi kupatwa na ugonjwa wa Corona.
Kwa upande wake Mratibu wa Afya kwa Umma Mkoa wa Mwanza Dokta Denis Kashaija alisema pamoja na kundi la Watoto kutopatiwa Chanjo lakini elimu inaendelea kutolewa mashuleni kuhakikisha tahadhari zote za kupambana na ugonjwa wa Corona zinafuatwa ikiwemo watoto kunawa mikono na maji tiririka,kuwepo kwa masanduku ya huduma ya kwanza pamoja na kusisitiza uvaaji barakoa.
Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Daktari Rutachinzibwa aliwataka wakazi wajiji la Mwanza wenye sifa ya kupatiwa chanjo hii ya awamu ya kwanza kuanza kujisajiri kwaajili ya kupatiwa chanjo hiyo itakayoanza kutolewa mwezi huu wa nane mwaka huu.

Dkt Rutachinzibwa alisema wananchi hawatakiwi kuwa na wasiwasi kuhusiana na chanjo hii kwa kuwa ni salama na kuwataka wananchi kuiamini serikali na wataalamu wake kwa kuwa hakuna serikali iliyotayari kuwaua wananchi wake.

”Hayo mauzi ambayo yanasemwa yapo katika dawa karibia zote na madhara yake ni madogo sana na hata ukiangalia asilimia kubwa ya waliochanjwa wapo salama hawajapata matatizo yoyote kwa maana hiyo ni waombe wote tukachanje chanjo”alisema Dkt Rutachinzibwa.
Timu ya Uhamasishaji wa Afua za Afya Mkoa wa Mwanza imeanza kukutana na makundi mbalimbali ya jamii kwa lengo la kutoa elimu juu ya umuhimu wa chanjo ya kupambana na Uvico 19 iliyoanza kutolewa hapa nchini.
Na Tonny Alphonce, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.