LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenyekiti APC awapongeza Wanahabari wa Mtandaoni

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), Claude Gwandu amewapongeza waandishi wa habari wa mtandaoni (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuitetea jamii.

Gwandu aliyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao cha tathmini ya mradi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu (Data Driven Advocacy- DDA) kwa mwaka 2020/21 kilichoambatana na upangaji mikakati ya utekelezaji kwa mwaka 2021/22.

Alisema waandishi hao baada ya kujengewa uwezo wamesaidia kuibua changamoto mbalimbali ya kijamii na kupitia majukwaa yao ya kihabari, zimekuwa zikipatiwa ufumbuzi. Aidha Gwandu aliwapongeza waandishi hao kwa kuendelea na majukumu yao hata wakati wa janga la Corona na kuhimiza waendelee kuchukua tahadhari wakati wakitimiza shughuli zao.

Katika hatua nyingine Gwandu alisema waandishi hao wa mtandaoni kupitia mradi wa DDA wamesaidia kuhimiza kufanyika kwa mabadiliko ya Sheria na Kanuni mbalimbali ikiwemo EPOCA ambazo zilikuwa zikilalamikiwa na wadau wa habari kuwa zinaminya uhuru wa habari ambapo katika hilo pia aliwashukuru viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari na Idara ya Habari Maelezo kwa ushirikiano wao mkubwa.

Naye Mwenyekiti wa waandishi wa habari mtandaoni kupitia mradi wa DDA, Midraj Ibrahim alisema wataendelea kufanya kazi ya utetezi wa masuala mbalimbali ikiwemo haki za binadamu kwani wajamii wanawategemea.

Mradi wa Utetezi Haki za Binadamu kwa kutumia Takwimu (DDA) unafadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka jana 2018 ambapo kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) unasimamiwa na UTPC kupitia APC.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa APC, Claude Gwandu akizungumza wakati wa kikao hicho.
Waandishi wa mtandaoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa APC, Claude Gwandu wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa DDA, Midraj Ibrahim akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa DDA, Midraj Ibrahim (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Mwanahabari Editha Karlo (katikati) kutoka Michuzi Blog mkoani Kigoma akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Mwanahabari Asha Shaban kutoka Jicho Letu Mara mkoani Mara akiwa kwenye kikao hicho.
Wanahabari wa mtandaoni wakiwa kwenye kikao hicho.
Wanahabari wa mtandaoni George Binagi kutoka BMG Online jijini Mwanza (kulia) na Asha Shaban kutoka Jicho Letu Mara (kushoto) wakijadiliana wakati wa kikao hicho.
Washiriki wa kikao hicho wakiendelea na majadiliano.

No comments:

Powered by Blogger.