LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bugando wana jambo lao kuelekea miaka 50 tangu kuanzishwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Hospitali ya Kanda Bugando iliyopo jijini Mwanza Ijumaa Agosti 06, 2021 inazindua maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake ambapo shughuli na huduma mbalimbali zitatolewa kwa wananchi katika kuelekea kilele cha maadhimisho hayo Novemba 03, 2021.

Tangu kuanzishwa kwake Novemba 03, 1971, Hospitali hiyo inajivunia utoaji huduma mbalimbali za afya hususani huduma za kibingwa huku ikiwa na mashine za kipekee ikiwemo mashinde ya kuchakata vivimbe mbalimbali vilivyotolewa mwilini (Kedee Tissue Processor), darubini kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo (Multheaded Microscope), mashine ya uchunguzi wa kemia na homoni (COBAS 6000) na nyinginezo nyingi.

Uzinduzi wa maadhimisho hayo pia unaambatana na utoaji huduma ya chanjo ya UVIKO 19 (COVID 19) kwa wafanyakazi, wazee na wenye magonjwa sugu huku yakiambatana na kaulimbiu isemayo “Tumepiga hatua, Tunathamini Afya Yako, Kazi Iendelee”.
Hospitali ya Kanda Bugando ambayo ujenzi wake ulianza mwaka 1968 inamilikiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na kuendeshwa kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere alifungua rasmi Hospitali hiyo Novemba 03, 1971 ikiwa na uwezo wa kuhudumia takribani mikoa minane ya Kanda ya Ziwa ambapo hadi kufikia mwaka 2017 ilihudumia watu milioni 14.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mwanza Robert Gabriel (hayupo) amewakilishwa na Mkuu Wilaya Nyamagana Amina Makilagi (wa pili kulia). Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Bugando, Dkt. Fabian Massaga.
Viongozi mbalimbali meza kuu akiwemo Mkuu wa Wilaya Nyamagana Amina Makilagi (wa pili kulia), Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mwanza Renatus Nkwande (wa kwanza kulia), Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Flavian Kassala (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Bugando Dkt. Phabian Massaga (wa pili kushoto).
Baadhi ya wananchi na wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando.
Uzinduzi wa Miaka 50 ya Bugando (Bugando Medical Centre Anniversary 1971-2021).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

No comments:

Powered by Blogger.