Jenerali Ulimwengu azindua Kitabu chake jijini Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwanahabari Mkongwe na Nguli nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu amezindua kitabu chake kiitwacho Rai ya Jenerali chenye maudhui ya makala alizoandikwa mwaka 1996 zinazoaksi masuala mbalimbali ikiwemo siasa na uongozi.
Akizungumza Septemba 21, 2021 kwenye uzinduzi huo jijini Mwanza, Ulimwengu alisema kitabu hicho kinatoa taswira ya masuala yanayoonekana sasa ambayo aliyaandika miaka mingi iliyopita na kwamba kitawasaidia wasomaji kuelewa vyema masuala hayo ambayo yanatokea sasa.
“Rai imejaa haja ya kuheshimu hoja siyo kupiga kelele, pili haja ya kuheshimu maoni. Tunaishi katika utamaduni wa kupigana vita na maoni ya watu, hatuwezi wote kuwaza kwa njia moja tukatapa maendeleo, lazima tuheshimu maoni ya wote” alisema Askofu Bagonza na kuongeza;
“Moja ya hoja za Jenerali Ulimwengu ni haja ya Katiba Mpya ambapo kwenye haja hii tumegawanyika kama nchi na kuna makundi makubwa manne. Kundi la kwanza ni wale wanaohitaji kuandika Katiba Mpya, kundi la pili ni lile linalosema tufanye marekebisho ya Katiba iliyopo, la tatu linasema vyote tuachane navyo kwamba kusiwe na Katiba Mpya wala marekebisho. Na kundi la nne ni wale wasiojua wanataka nini na wengi wako vijijini. Hivyo ni wajibu wenu kuelimisha hilo ili kujua linataka nini” alidokeza Askofu Bagonza.
Wadau malimali wakifuatilia uzinduzi wa kiabu hicho.
Nakala ya Kitabu cha Rai ya Jenerali inauzwa shilingi elfu 30.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari zaidi hapa
No comments: