LIVE STREAM ADS

Header Ads

NACOPHA watoa mafunzo ya ufuatiliaji wanaoishi na VVU

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU (NACOPHA Kanda ya Mwanza) limetoa mafunzo ya siku mbili kuhusu ufuatiliaji wa upatikanaji wa huduma za watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI katika jamii.

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, Afisa Ufundi NACOPHA, Joseph Bukula amewataka washiriki hao kuhakikisha wanaelewa lengo la mafunzo hayo ili waweze kuwasaidia watu wanaoishi na VVU katika maeneo yao ili kupata huduma bora katika vituo vyote vya afya vinavyowazunguka sambamba na kuwa na takwimu sahihi za WAVIU.
Mafunzo hayo yaliyotolewa na NACOPHA kupitia mradi wa HEBU TUYAJENGE unaofadhiliwa na shirika la USAID na kuwashirikisha wadau kutoka mabaraza ya WAVIU (Konga) na Waratibu wa Konga kutoka Halmashauri za Nyamagana, Shinyanga, Musoma na Sikonge.

No comments:

Powered by Blogger.