LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya NMB yaahidi makubwa kwa waalimu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya NMB imewaahidi waalimu ushirika wa uhakika katika utoaji wa huduma mbalimbali ikiwemo mikopo ya ujenzi wa nyumba, mikopo ya biashara na Bima ikiwa ni ushirikiano wenye faidha baina ya NMB na waalimu.

Hayo yalisema na Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu NMB, Emmanuel Akonaay wakati akitoa salamu kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani 2021 yaliyoadhimishwa kwa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita katika uwanja wa Shule ya Sekondari Ushirombo.

Akonaay alisema waalimu wamekuwa washirika wakubwa wa benki ya NMB hivyo benki hiyo itaendelea kuwa karibu nao kwa kuhakikisha wanapata huduma bora masaa 24 kupitia mtandao mpana ulioenea nchi nzima pamoja na njia ya kidijitali ya NMB Mkononi.

Katika kudhihirisha ushirika baina ya benki ya NMB na waalimu, benki hiyo ilidhamini mashindano ya ligi ya waalimu wilayani Bukombe ya Mwalimu Doto Cup 2021 yaliyoasisiwa mwaka 2019 na Mbunge wa Bukombe Dkt. Doto Biteko kwa kutoa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo jezi, mipira na medali vyenye thamani ya shilingi milioni 14.5.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Magesse (kushoto) akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani 2021 yaliyofanyika kwa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita katika uwanja wa Shule ya Sekondari Ushirombo. Kulia ni Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu NMB, Emmanuel Akonaay.
Viongozi mbalimbali meza kuu akiwemo Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt. Doto Biteko (kulia), Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Magesse (kushoto) na Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu NMB, Emmanuel Akonaay (katikati).
Wadau mbalimbali waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani 2021 katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
Waalimu kutoka Kata 17 za Wilaya ya Bukombe wakifuatilia Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani yaliyofanyika Oktoba 05, 2021 yakiambatana na utoaji zawadi kwa washindi wa ligi ya waalimu ya Mwalimu Doto Cup 2021.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.