LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwitikio wa chanjo ya Corona waendelea kuongezeka

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Takribani watu elfu 28 wamefanikiwa kuchanjwa chanjo ya Corona mkoani Mwanza.
Akizungumza kwenye mdahalo waandishi wa habari, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Thomas Rutachunzibwa amesema mwitikio umekuwa mkubwa tofauti na mwanzo.

Amesema awali wakati chanjo inaanza walikuwa wakichanja watu 200 na hadi sasa wanafikia 1,600 kwa siku. Aidha amesema maeneo ya vijijini yamekuwa na mwitikio mkubwa kuliko mijini na kwamba vituo 346 ziko wazi kwa ajili ya huduma hiyo.

"Mwanzoni tulikuwa na vituo 27 lakini kwa sasa tuna vituo 346 na chanjo hii haina madhara kiafya" amesema Rutachunzibwa na kuongeza kuwa lengo la Serikali ni kufikia asilimia 60 ya watu waliochanjwa nchini.
Na Annastazia Maginga, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.