Waziri Biteko awataka wafanyabiashara Mwanza kuhamia kwenye soko jipya
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amewataka wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza (Dealers & Brokers) wenye ofisi katika jengo la Rock City Mall kuhamia katika soko jipya la madini lililopo katika eneo la Pasiansi kilipo kiwanda cha kusafisha madini Mwanza (MPMR).
Waziri Biteko ameyasema hayo Oktoba 11, 2021 wakati wa kikao baina yake na wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza huku akiongeza kuwa angetamani kuona zoezi hilo linakamilika ndani ya wiki mbili.
Katika hatua nyingine Waziri Biteko amebainisha kuwa baada ya Serikali kupata usajili (Certification) za viwanda vya kusafisha dhahabu vilivyopo Mwanza, Geita na Dodoma itazuia usafirishaji wa dhahabu ambayo haijasafishwa (ghafi) nje ya nchi hivyo wafanyabiashara wajiandae na mabadiliko hayo.
Aidha Waziri Biteko amewahakikishia wafanyabiashara na wachimbaji wa madini kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu inafanya kila jiihada ili kuhakikisha wananufaika na biashara ya madini hivyo ni wakati wao kuchangamkia fursa hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Sengerema, Senyi Ngaga akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa Mwanza, Robert Gabriel kwenye kikao hicho.
Wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: