LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kampuni ya Barrick yaanzisha maabara ya kwanza ya 'Chrysos Photon Assay' barani Afrika

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukuru Manya (wa tatu kulia), Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow (wa pili kulia) wakikata utepe kuzindua maabara ya kisasa ya kupima madini katika mgodi wa Bulyanhulu. Kulia ni mjumbe wa bodi ya Twiga Mineral,Casmir Kyaki.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow akimwonyesha Naibu Waziri wa Madini,Profesa Shukuru Manya ramani ya mgodi wa Bulyanhulu wakati wa hafla ya kuzindua maabara ya kisasa ya kupima madini katika mgodi wa Bulyanhulu.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow (kulia) akiongea na Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukuru Manya wakati wa hafla ya uzinduzi wa maabara ya kisasa ya Bulyanhulu.
Wageni walioshiriki hafla ya uzinduzi wa maabara ya kisasa ya kimataifa wakibadilishana mawazo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick ,Mark Bristow na Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukuru Manya.

Na Kadama Malunde, Shinyanga
Kampuni ya Dhahabu ya Barrick, kwa kushirikiana na kampuni ya MSALAB Ltd, zimefanikiwa kuanzisha katika mgodi wa Bulyanhulu nchini Tanzania maabara ya kisasa inayotumia mtambo wa Chrysos Photon Assay kupima kiwango cha madini kwa eksirei. Maabara hii ni ya kwanza na ya aina yake barani Afrika na katika uendeshaji wa shughuli za Barrick duniani.

Mbinu hii mpya inatoa uchambuzi wa haraka,salama na sahihi zaidi wa madini ya dhahabu, fedha na elementi nyinginezo za ziada kwa kutumia kipimo kisichoharibu mazingira cha sampuli kubwa na wakilishi zaidi ndani ya dakika mbili tu, jambo linalowezesha mabadiliko ya haraka katika suala la taarifa muhimu za uendeshaji wa shughuli za kampuni ambazo zinachochea ufanisi wa hali ya juu kabisa katika mnyororo mzima wa thamani katika uchimbaji madini.

Mfumo huu unaleta mbadala endelevu zaidi wa njia za jadi za kutumia moto ambao si rafiki kwa mazingira,usiotumia kemikali na hivyo,unapunguza wa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa ya ukaa na taka hatarishi.

Akiutambulisha mfumo huo mpya kwa vyombo ya habari kwenye mgodi wa huo, Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, amesema kuwa hiyo ilikuwa sehemu ya jitihada endelevu za kampuni za kutaka kutumia uvumbuzi wa kiteknolojia katika kuhakikisha kwamba shughuli zake zinaendeshwa kwa umahiri,kunakuwa na usalama na usalama kazini na mazingira yanatunzwa vizuri.

No comments:

Powered by Blogger.