LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kahama Jogging wajiandaa kuwakabili Shinyanga Jogging

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kuelekea Mashindano ya Michezo mbalimbali itakayofanyika uwanja wa Manispaa Kahama Jumapili ya Oktober 17, 2021 Klabu ya mazoezi ya Kahama Jogging imeanza maandalizi ya kuwakabili wenzao wa Klabu ya michezo kutoka Shinyanga itwayo Shinyanga Jogging.


Akiongea na Kahama Fm Oktoba 10, 2021 baada ya mazoezi, Mwenyekiti wa Kahama Jogging Hussen Salumu amesema kuwa Kahama Jogging imejipanga kushinda michezo yote kwani washiriki wamejitoa kwa moyo wote kuhakikisha wanashinda katika michuano hiyo.


Salumu amesema kuwa wanawatambua Shinyanga Jogging kwa muda mrefu na kwamba mashindano ya Jumapili wasitegee ushindi wowote kwani mazoezi wanayoendelea nayo ni makali yakuhakikisha ushindi unabaki Kahama.
Akielezea mazoezi yaliyofanyika hayo, Katibu wa Kahama Jogging Yusuph Makombe amesema kuwa leo wamekimbia umbali wa km 10 kukimbia kwenye magunia na kuvuta kamba sanjali na kufanya mazoezi ya viungo.


Nao baadhi ya wanachama wa Kahama Jogging, Steve Cleophace na Lubango Yusuph wamesema kuwa wamejipanga vizuri kushindana na Shinyanga Jogging na kwamba mazoezi yote wanayotolewa na walimu wanayazingatia huku wakitoa salamu kwa wapinzani wao kujiandaa kikamilifu.
Kahama Jogging inatarajia kuwakaribisha Shinyanga Jogging siku ya jumapili Oktober 17, 2021 katika uwanja wa Manispaa Kahama kushindana michezo mbalimbali ikiwemo mbio za kawaida na mbio za magunia, kuvuta kamba, mpira wa miguu, mpira wa pete pamoja na michezo mingine.

No comments:

Powered by Blogger.