LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenge wa Uhuru watua wilayani Mbogwe, Geita

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenge wa Uhuru umewasili katika Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita ambapo unatarajiwa kukimbizwa kilomita 185.7 na kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kukagua utekelezaji wake, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi iliyokamilika.

Mapokezi ya Mwenge huo yamefanyika Oktoba 10, 2021 katika uwanja wa Lulembela ukitokea wilayani Bukombe ambako ulikagua na kupitisha miradi yote 10 wilayani humo ikiwemo mradi wa maji Busanzu pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuongeza thamani mazao ya nyuki Buombe.

Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini walishiriki kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Bukombe.
Mkuu wa Wilaya Mbogwe, Mhandisi Charles Kabeho akipokea Mwenge wa Uhuru Oktoba 10, 2021.
Mkuu wa Wilaya Mbogwe, Mhandisi Charles Kabeho akipokea Mwenge wa Uhuru.
Viongozi mbalimbali wilayani Bukombe wakiteta jambo baada ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru wilayani Mbogwe.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.