LIVE STREAM ADS

Header Ads

UWT Mwanza watoa msaada Sekou Toure, waahidi Mitano Tena kwa Rais Samia 2025

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa Mwanza Oktoba 11, 2021 umekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo sababuni, taulo za kike, vyandarua na mashuka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Wiki ya UWT 2021. 

Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi mahitaji hayo, Mwenyekiti wa UWT Mkoa Mwanza, Hellen Bogohe amempongeza Rais Samia kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na uboreshaji wa sekta ya afya ikiwemo kutoa mashine ya CT Scan katika Hospitali ya Sekou Toure na kueleza kuwa zawadi watakayompa ni kumuongeza miaka tena katika uchaguzi wa mwaka 2025.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa UWT Mkoa Mwanza, Hellen Bogohe akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya UWT 2021.
Mganga Mkuu Mkoa Mwanza, Dkt. Thomas Ruttachunzibwa akitoa shukurani baada ya kupokea msaada wa mahitaji mbalimbali kutoka UWT Mkoa Mwanza ambapo aliahidi mahitaji hayo kutumika kwa walengwa ambao ni akina mama hospitalini hapo.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure, Dkt. Bahati Msaki akitoa taarifa ya Hospitali hiyo jinsi ilivyoboresha huduma za mama na mtoto ikiwemo uwepo wa chumba maalum cha upasuaji pamoja na ujenzi wa jengo jipya la mama na mtoto lengo likiwa ni kuzuia kabisa vifo vitokanavyo na uzazi.
Wanawake wa UWT Mkoa Mwanza.
Wanawake wa UWT Mkoa Mwanza pia walipata fursa ya kuchanjwa chanjo ya UVIKO 19.
Mahitaji mbalimbali ikwemo sabuni pamoja na taulo za kike yaliyokabidhiwa katika Hospitali ya Rufaa Sekou Toure kwa ajili ya kuwasaidia akina mama waliojifungua hospitalini hapo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya UWT 2021.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.