LIVE STREAM ADS

Header Ads

RUWASA waendelea kuchapa kazi Musoma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com 
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Musoma mkoani Mara, Edward Sironga akizungumzia miradi ya maji inayotekelezwa wilayani humo.

Na Shomari Binda, Musoma
Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) katika Wilaya ya Musoma mkoani Mara imesema kazi ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji wilayani humo inaendelea kwa kasi ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Akizungumza na Waandushi wa Habari Kijiji Cha Wanyere Kata ya Suguti, Meneja wa Ruwasa wilayani Musoma, Edward Sironga alisema kazi ya kuunganisha miundombinu ya maji inaendelea vyema na kwamba tayari wamewasiliana na wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili kupata ridhaa ya kupitisha mabomba katika maeneo ambayo yanakatisha barabarani.

Sironga amesema wameshaandika barua Tanroads kuhusiana na hilo na litakapokamilushwa kazi zitaendelea.

" Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suruhu Hassan, tumepewa zaidi ya bilioni 8 kutekeleza miradi ya maji.

' Tunashukuru pia mbunge wa jimbo la Musoma vijijini,Profesa Sospeter Muhongo,kwa jitihada zake za kuwafikishia wananchi huduma",amesema Sironga.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Suguti  wameshukuru kwa kufikishiwa huduma ya maji wakati kipindi cha nyuma walifata zaidi ya kilometa 15.

No comments:

Powered by Blogger.