Bodaboda kusaidia mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela pamoja na Jeshi la Polisi Wilaya Ilemela, limezindua kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia wilayani Ilemela.
Akizungumza Ijumaa Novemba 05, 2021 wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini Yassin Ally alisema kampeni hiyo inalenga kuwashirikisha bodaboda kama Wakala wa Mabadiliko katika kutokomeza tatizo la mimba pamoja na ndoa za utotoni kufuatia baadhi yao kudaiwa kuwa chanzo cha tatizo hilo.
Aliongeza kuwa kampeni hiyo inalenga kuwafanya bodaboda kujitambua katika malengo yao binafsi ya maisha pamoja na kuchangia katika maendeleo ya taifa ikiwa ni pamoja na kuwa mabalozi wazuri wa kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Ally aliendelea kusisitiza kuhusu Kauli mbiu ya 'Chapa Kazi Siyo Mkeo na Kama Unapenda Sketi za Shule, Mshonee Mkeo', Funguka! Muwezeshe asome usimpe mimba'.
Akizindua kampeni hiyo,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga aliwataka waendesha bodaboda kuzingatia kanuni,taratibu na sheria katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja kuwa waadilifu katika maisha yao ya kila siku huku wakiwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia.
Mulunga aliwaasa waendesha bodaboda kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na manispaa hiyo pamoja na kujiwekea akiba ili kupata mitaji ya kuwekeza kwenye shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato.
Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wa wilaya Ilemela Mrakibu mwandamizi wa polisi Elisante Ulomi aliwatahadharisha waendesha bodaboda wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.
Ulomi aliwaasa waendesha bodaboda kuwafichua wanaojihusisha na mapenzi na wanafunzi ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Nao baadhi ya waendesha bodaboda walikiri baadhi yao kujihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kukwapua mikob ya abiria hususani wanawake pamoja na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.
Aidha waliiomba serikali kukomesha uwepo wa wimbi la waendesha bodaboda wasiokuwa na vituo maalum ambao wamedai kuwa vinara wa uhalifu pamoja na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.
Pia waliomba Shirika la Kivulini liwapatie elimu ya kujitambua mara kwa mara ili waweze kuwa mabalozi wema zaidi wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia.
Waendesha bodaboda 135 kutoka kata mbalimbali za manispaa ya Ilemela zikiwemo Buswelu, Nyamhongolo na Kahama walipatiwa viakisi mwanga (Reflectors) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza ambapo mratibu wa sekta isiyo rasmi katika manispaa hiyo Raphael Mfuru amewahimiza kuzitumia kwa malengo yaliyokusudia ili kuleta matokeo chanya.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela. Katikati ni Mkuu wa polisi wilaya Ilemela Mrakibu Mwandamizi wa polisi Elisante Ulomi , kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela. Katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally , kulia ni Mratibu wa Sekta isiyo rasmi manispaa ya Ilemela Raphael Mfuru.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally akitoa mafunzo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Mratibu wa sekta isiyo rasmi halmashauri ya manispaa ya Ilemela Raphael Mfuru akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilayaIlemela Celestine Lusendelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Imeandaliwa na Malunde 1 Blog
No comments: