LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko aonya kufunga mgodi Bunda, atoa siku saba

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko ameonya kuyafunga machimbo ya dhahabu ya Kinyambwiga yaliyopo katika Wilaya Bunda mkoani Mara ikiwa wamiliki wa mashamba pamoja na wamiliki wa leseni za uchimbaji madini hawatamaliza mgogoro walionao.

Dkt. Biteko ametoa onyo hilo Disemba 28, 2021 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika machimbo hayo huku pia akipiga marufuku wamiliki wa mashamba kuwatoza wenye maduara shilingi laki tano ndipo wawaruhusu kufanya shughuli za uchimbaji.

Waziri Dkt. Biteko ametoa muda wa majadiliano hadi kufikia Januari 07, 2022 wahusika wawe wamemaliza mgogoro uliopo ambao umedumu takribani miezi minne na hivyo kuathiri shughuli za uchimbaji kwa wenye madualra na kuongeza kuwa ikiwa mwafaka hautafikiwa atayafunga machimbo hayo kwa mujibu wa Sheria.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Bunda, Joshua Nasary akitoa salamu kabla ya kumkaribisha Waziri Biteko kuzungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Kinyambwila.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko na msafara wake alipotembelea machimbo ya Kinyambwiga wilayani Bunda.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na viongozi mbalimali akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mara Samwel Kiboye (wa kwanza kushoto) kukagua machimbo ya dhahabu ya Kinyambwila wilayani Bunda.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.