LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Biteko awasimamisha watumishi saba, awaonya vikali watatu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amemwagiza Kaimu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba kuwasimamisha kazi watumishi saba kutoka mikoa ya kimadini ya Geita, Mbogwe na Kahama kutokana na tuhuma za rushwa na wizi kazini.

Aidha ametoa onyo kali kwa watumishi wengine watatu kutoka mikoa ya kimadini ya Kahama na Kagera ambao wamekuwa si waadilifu wakigubikwa na malalamiko lukuki kutoka kwa wachimbaji pamoja na wafanyabiashara wa madini.

Dkt. Biteko amechukua maamuzi hayo mazito Disemba 22, 2021 wakati akizungumza kwenye kikao baina yake na wafanyabiashara wa madini pamoja na Maafisa Madini Wakazi kutoka mikoa ya kimadini ya Kanda ya Ziwa kilichofanyika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. 
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko (kulia) pia alitembelea soko la dhahabu la Kahama kukagua uendeshaji wake.
Wafanyabiashara wa madini kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakimsikiliza Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko alipokutana nao wilayani Kahama.
Mbunge wa Jimbo la Msalala wilayani Kahama akitoa salamu kwenye kikao cha Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko na wafanyabiashara wa madini Kanda ya Ziwa.
Mmoja wa wafanyabiashara akieleza jambo kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Sophia Mjema akitoa salamu za mkoa kwenye kikao hicho ambapo aliahidi kusimamia vyema masuala yote ya kiusalama ili kuhakikisha biashara ya madini inafanyika vyema mkoani Shinyanga.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akizungumza na wafanyabiashara wa madini Kanda ya Ziwa kwenye kikao ambacho kilihudhuliwa pia na Maafisa Madini kutoka mikoa 11 ya kimadini Kanda ya Ziwa.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akizungumza kwenye kikao hicho.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akizungumza kwenye kikao hicho ambapo pamoja na mambo mengine aliwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wasio waadilifu.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia kikao hicho.
Wafanyabiashara wa madini kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia kikao hicho.
Wafanyabiashara wa madini wakiwa kwenye kikao hicho.
Watumishi mbalimbali kutoka Wizara ya Madini wakifuatilia kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya Kahama Festi Kiswaga akitoa salama kwenye kikao hicho.
Wafanyabiashara wa madini kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini wakati Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko (hayuko pichani) akiwasili.
Wafanyabiashara wa madini kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini.
Wafanyabiashara wa madini kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini wakati Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko (hayuko pichani) akiwasili.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko (kushoto) akiwasili kwenye kikao baina yake na wafanyabiashara wa madini kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kilichofanyika wilayani Kahama.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Biteko kazini

No comments:

Powered by Blogger.