Baraza la UVCCM Nyamagana lampongeza Rais Samia
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, limepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoiongoza vyema nchi pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2020/25.
Akisoma maazimio ya Baraza hilo kwenye kikao kilichofanyika Disemba 22, 2021. Katibu wa UVCCM Wilaya Nyamagana Malanyingi Matukuta alisema Rais Samia amekuwa kiongozi wa kuonesha dira ya Serikali anayoiongoza kwa kuzingatia uadilifu, utawala wa sheria, haki, usawa, mshikamano na kuimarisha demokrasia.
Alisema Rais Samia ametoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi mipya na kuendeleza miradi iliyokuwepo.
Wajumbe wa Baraza la UVCCM Wilaya Nyamagana.
Soma hapa chini maazimio kamili ya Baraza la UVCCM Wilaya Nyamagana wakimpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
SOMA>>> Habari zaidi kuhusiana na UVCCM
No comments: