LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mahafali ya 11 Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi (CDTTI) Misungwi yafana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wahitimu 356 wamehitimu masomo yao na kutunukiwa Astashahada na Stashahada mbalimali ikiwemo Uhandisi Ujenzi na Maendeleo ya Jamii katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi (CDTTI) mkoani Mwanza.

Hafla ya kuwatunuku wahitimu hao imefanyika Ijumaa Disemba 10, 2021 kwenye kusanyiko la Mahafali ya 11 ya Chuo hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya Magu Salum Kalli.
Mwonekano wa majengo mbalimbali katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi mkoani Mwanza.
Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi wameajiriwa na kujiajiri katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi wakiwa kwenye Mahafali ya 11 mwaka huu 2021.
Viongozi na watumishi mbalimbali wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi.
Viongozi mbalimbali meza kuu wakiwa kwenye Mahafali ya 11 Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi.
Viongozi mbalimbali meza kuu wakifuatilia mahafali hayo.
Wahitimu Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi pamoja na waalimu wao wakifurahia kwenye mahafali ya 11 ya Chuo hicho Disemba 10, 2021.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Magu Salum Kalli (katikati) akiwa kwenye Mahafali hayo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (hayuko pichani). Kuhsoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi Charles Achuodho na kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza Isack Ndasa ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi.
Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi wakiwasili kwenye viunga vya Chuo hicho kwa ajili ya kusanyiko la Mahafali ya 11 ya Chuo hicho yaliyofanyika Disemba 10, 2021.
Wahitimu wakiwasili kwenye mahafali.
Wahitimu na wanachuo wakiwasili kwenye kusanyiko.

Mgeni rasmi akiwasili kwenye kusanyiko.
Mgeni rasmi akikagua maonesho mbalimbali ya kitaaluma.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi upande wa Taaluma, Mwl. Dongo Nzori (wa pili kulia) akifurahia pamoja na wahitimu wa chuo hicho. 
Wahitimu wakiwemo mafunzo ujenzi ngazi ya jamii wakipokea vyeti baada ya kuhitimu mafunzo katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.