LIVE STREAM ADS

Header Ads

UTALII WA JIOLOJIA NDANI YA BANDA LA GST WAWAVUTIA WATANZANIA WENGI VISIWANI ZANZIBAR KATIKA MAONESHO YA SITA YA VIWANDA NA BIASHARA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Na Samwel Mtuwa, GST
Ikiwa ni kilele cha sikukuu ya miaka 60 ya Uhuru zilizoambatana na maonesho maalum ya kitaifa ya viwanda na Biashara yakiwa na lengo la kuimarisha bidhaa za Tanzania na kujenga uchumi wa Tanzania Bara na visiwani.

Katika maonesho hayo ndani ya Banda la GST wananchi wamefurahishwa na maelezo ya kina juu ya elimu ya Jiolojia yaliyokuwa yakitolewa kupitia ramani maalum ya Utalii wa Jiolojia iliyoandaliwa na GST Kwa lengo la kukuza Utalii wa Jiolojia nchini.

Sambamba na maelezo juu ya Utalii wa Jiolojia wananchi waliotembelea Banda la GST walipata elimu hatua zilizofikiwa katika  tafiti za madini nchini kwa kipindi cha  kabla na baada ya Uhuru mwaka 1961.

Pamoja na maelezo hayo ya maendeleo ya Utafiti wa Madini nchini, wananchi wamepata ufahamu  juu ya hatua mbalimbali za  Utafutaji , Uchunguzi na uchenjuaji Madini.
Maonesho hayo yamefungwa rasmi na Omar Shabaan ambaye ni Waziri wa Biashara , Maendeleo na Viwanda katika Serikali ya Zanzibar.

Kwa mwaka huu 2021 maonesho haya yameshirikisha washiriki 113 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

No comments:

Powered by Blogger.