LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maonesho ya Wajasiriamali Afrika Mashariki yaongeza tija kwa jamii

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Judith Ferdinand, Mwanza
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amesema asilimia 90 ya mapato ya biashara zinazofanywa na wajasiriamali wanawake yanarudi kusaidia familia na kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo chakula,matibabu na elimu.

Ameongeza kuwa mapato hayo pia ni fursa ya kuvunja umasikini na kuwapa wanawake nafasi ya kufanya biashara huku tafiti zikionesha mapato ya wanaume ni chini ya asilimia 50 na kuhoji zaidi ya asilimia 50 yanakwenda wapi.

Prof. Mkumbo alitoa kauli hiyo Disemba 05, 2021 wakati akifungua maonesho ya 21 ya wajasiriamali wadogo na wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama Nguvu Kazi/Jua Kali yanayofanyika Rock City Mall mkoani Mwanza ambapo alimwakilisha Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Maonesho hayo yamebeba kauli mbiu ya "Ukuzaji ubora na ubunifu ili kuinua ushindani wa ujasiriamali wadogo wa Afrika Mashariki na ahueni baada ya UVIKO-19” ambapo yalianza Desemba 02-12 mwaka huu.

Alisema asilimia 6O ya washiriki katika maonesho hayo ni wanawake hivyo mapato yao yataenda kusaidia katika familia zao katika masuala ya chakula, matibabu na elimu ya watoto hivyo mapato hayo ni fursa ya kuvunja mnyororo wa umasikini.

"Maonesho haya yana umuhimu mkubwa kwani nchi zote duniani ujasiriamali unachukua nafasi kubwa ,naomba nisahihishe hapa hakuna mfanyabiashara mdogo kuna biashara ndogo na biashara ya kati” alisema Prof. Mkumbo.

Kuhusu wajasiriamali Prof. Mkumbo alisema vijana ndio matajiri wakubwa watarajiwa ambao kwa upande wa Tanzania wamefanya utafiti wa viwanda na biashara uzalishaji bidhaa asilimia 98 unatokana na viwanda vidogo sana na vidogo.

Akizungumzia suala la kuwawezesha wajasiriamali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Prof. Mkumbo alisema serikali zote za nchi hizo zimekubaliana kuwa na sera moja za kuendeleza wajasiriamali wadogo na wa kati.

Pia wataendelea kufanya kazi ya kuondoa vikwazo vinavyo kwamisha wafanyabiashara katika Jumuiya hiyo.

"Tuwaunge mkono viongozi wetu,ambao ambao wamepanga kuona mazingira ya kufanyia biashara yana kwenda kuboreshwa , wajasiriamali kuweni wabunifu ambao ubunifu huo pia tumeuona kwa wajasiriamali wetu katika maonesho haya" alisema Prof. Mkumbo.

Aidha alisema lengo la Serikali ni kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati ili wazalishe bidhaa za kutosheleza mahitaji ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Tumeona namba kubwa ya wanawake na vijana wamejitolea kuzalisha bidhaa za ubunifu, serikali itahakikisha inawekeza nguvu katika uwezeshaji wao ili kuhakikisha viwanda vyetu vinapata malighafi ya kutosha inayozalishwa na wazalishaji wadogo na wa kati" alisema Prof. Mkumbo.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wajasiriamali wa Jumuiya ya aAfrika Mashariki, Josephat Rweyemamu alisema maonesho hayo yalianza mwaka 1999 yakiwa na washiriki 59 Sasa wameongezeka Hadi kufikia takribani wajasiriamali 1400 pia bidhaa zimeongezeka na zingine zimepata nembo za ubora.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel alisema jumla ya wajasiriamali 1,304 wamethibitisha ushiriki kati ya hao 794 wametoka katika nchi za Kenya,Uganda,Sudan ya Kusini,Burundi,Rwanda na 510 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.

"Maonesho haya kwetu sisi kwa wanamwanza ni fursa ya kipekee ya kuandika historia ya Mkoa wetu wa Mwanza,yamesaidia kukua kwa pato la taifa na wajasiriamali, pia kupitia mzunguko wa fedha utasaidia Mkoa kuongeza pato" Mhandisi Gabriel alisema na kuongeza;

"Nindelee kutoa wito kwa wananchi wa Mwanza na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kujitokeza kutembelea mabanda na kununua bidhaa kwa kufanya hivyo tunainua uchumi wetu na kuendelea kutangaza bidhaa za wajasiriamali wa Jumuiya hii" alisema Mhandisi Gabriel.

Mhandisi Gabriel amesema kuwa Mwanza ni eneo lenye ardhi nzuri na uchumi ,kuna maeneo mbalimbali ya uwekezaji na yakibiashara hivyo wafanyabiashara wajitokeze kuwekeza.

Aliongeza kuwa hakuna rushwa wala kuzungushana katika upatikanaji wa maeneo huku akitia wito kwa wananchi kujitokeze kwa wingi katika maonesho hayo ili kukuza uchumi na kuzitangaza bidhaa mbalimbali za Afrika Mashariki.

Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Walemavu), Jenista Mhagama alisema tatizo la ajira ni kwa wote hivyo maonesho hayo ni ufunguo wa ajira, kukuza uchumi pia ni nyenzo ya kubadilishana ujunzi ambao unaweza kutengeneza ajira nyingi nchini pamoja na kubadilishana elimu ya ujasiriamali na kudumisha umoja na mshikamano.

"Maonesho haya yanaendana sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru na kuonesha thamani ya uwepo wetu,kutumia rasilimali tulizonazo,kutumia teknolojia na ujuzi kidogo lakini tukaboresha bidhaa,ambazo zinaweza kuingia kwenye masoko makubwa ya kimataifa" alisema Mhagama

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Wajasiriamali nchini Kenya David Osiany alisema anafarijika kuona akinamama na vijana wajasiriamali kwenye maonesho ya mwaka huu ambapo nchini Kenya sekta hiyo inachangia asilimia 83 ya ajira.

Amesema maonesho ya wajasiriamali yanatoa fursa kuonesha dunia kuwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki si watu wa kununua bidhaa za nje ya nchi zao bali wanao ujuzi wa kutengeneza bidhaa zenye ubora.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maonesho ya biashara ya wajasiriamali wa Afrika Mashari yanayofanyika jijini Mwanza.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Walemavu), Jenista Mhagama akitoa salamu za Wizara yake kwenye ufunguzi huo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akitoa salamu kwenye ufunguzi wa maonesho hayo.
Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa kwenye banda la Wizara hiyo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.
Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa kwenye Maonesho ya Wajasiriamali Wadogo na Wakati Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza.
Mwonekano wa mabanda mbalimbali kwenye Maonesho hayo.
Bidhaa mbalimbali za asili kwenye Maonesho hayo.
Wananchi wakitembelea mabanda mbalimbali.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mklumbo (wa pili kulia) akiteta jambo na viongozi mbalimbali baada ya ufunguzi wa maonesho hayo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Walemavu), Jenista Mhagama (wa tatu) akiteta jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (wa kwanza kushoto).
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kulia) akipokea picha kutoka kwa mmoja wa wabunifu walioshiriki maonesho ya wajasiriamali Afrika Mashariki.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akipokea picha kutoka kwa mmoja wa wabunifu walioshiriki maonesho ya wajasiriamali Afrika Mashariki.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akitembelea mabanda mbalimbali.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akivishwa vazi la asili na wajasiriamali kutoka nchini Sudan Kusini.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akifurahia jambo wakati akitembelea mabanda mbalimbali.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akiwa kwenye banda la TBC.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akijionea ubunifu wa wajasiriamali mbalimbali kwenye maonesho hayo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akijionea bunifu mbalimbali kwenye maonesho hayo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akifurahia biadhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali.
Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara.
Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Watumishi wa Wizara hiyo.
Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali meza kuu.
Viongozi mbalimbali meza kuu.
Wadau mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa maonesho hayo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza.
Burudani.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (katikati) akikabidhi hati za pongezi kwa wadau waliosaidia kufanikisha maonesho ya wajasiriamali Afrika Mashariki.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akitoa hati/ vyeti vya pongezi kwa waliofanikisha maonesho hayo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akimkabidhi cheti mmoja wa wadau waliofanikisha maandalizi ya maonesho hayo. 
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akikabidhi cheti cha pongezi kwa mmoja waliosaidia kuandaa maoenesho hayo.
Hongereni sana kwa kufanikisha maonesho ya wajasiriamali Afrika Mashariki 2021.
Pongezi kwa wote waliofanikisha maonesho hayo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akipokea picha kutoka kwa mbunifu wa uchoraji aliyechora picha yake na kumkabidhi kama zawadi.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akijionea picha kutoka kwa kijana mbunifu.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akimpongeza kijana mbunifu aliyechora picha yake.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.