LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake washiriki kwa wingi Maonesho ya Wajasiriamali Afrika Mashariki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Na Rebecca Luzunya, Mwanza
Mwitikio wa wanawake walioshiriki maonyesho ya wajasiriamali wadogo wa Afrika Mashariki yaliyozinduliwa Disemba 05, 2021 jijini mwanza umekuwa mkubwa ikilinganishwa na wanaume..

Maonyesho hayo ya 21 yanayozihusisha nchi sita za Afrika mashariki yamewakutanisha zaidi ya wajasiriamali wadogo na kati 1,304 kutoka katika nchi hizo.

Wanawake ni zaidi ya asilimia 60 ya washiriki katika maonyesho hayo huku wageni kutoka nchi mbalimbali wakiwa ni 794 na 510 kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania.

Akizungumzia muitikio huo wa wanawake, mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo, Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo alisema akina mama wakipewa nyenzo wanaweza kufanya mambo makubwa.

Mkumbo alisema wanawake wanauwezo mkubwa wa kufanya mambo pale wanapopata nafasi na anaimani kubwa asilimia 90 ya mapato wanayoyapata yanarudi katika familia.

Aliongezea kuwa maonyesho haya yanafanya vizuri kutokana na umoja wetu ingawa umoja huu unapaswa kuimarishwa zaidi ili tuweze kufikisha mbali umoja huu na hatimaye kuwajengea uwezo wafanyabiashara kuwakilisha bidhaa zao nje ya mipaka ya afrika mashariki.

"Tunapaswa kusimamia umoja huu kwa malengo na makusudio thabiti kama ambayo waasisi wetu walitarajia wakati wanaunda umoja huu" alisema mkumbo.

Maonyesho haya yanachangia kwa kiasi kikubwa kudumisha umoja, ushirikiano hali inayochangia kukuza biashara na uchumi wa jumuiya yetu.

Kwa upande wa Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema tuendelee kuenzi muunganiko huu wa kibiashara kama ulivyoundwa.

Amesema sasa kiu hii imeonekana kuwa kubwa kwa hiyo si vibaya hata yakifanyika mara mbili kwa mwaka.

"Biashara ndogo ni chanzo cha ongezeko la uchumi pia ni chanzo cha ajira kwa wananchi na inasaidia sana watu kujiajiri kutokana na changamoto ya ajira inayoikabili africa mashariki na hata dunia nzima" alisema Mhagama.

Alisema wananchi tuamke tuchangamkie fursa hizi ili tuweze kukuza uchumi wa nchi yetu na Uchumi wa mtu mmoja mmoja.

No comments:

Powered by Blogger.