LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakulima Tanzania waanza kunufaika na Teknolojia ya Kinyonga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Na Mwandishi Maalum, Iringa
Wakulima katika skimu za kilimo cha umwagiliaji Kiwere na Mafuruto, wamenufaika na teknolojia ya kisasa katika setka ya kilimo cha Umwagiliaji, ambayo ni mbadala wa matumizi ya rasimali maji,maarufu kwa jina la kinyonga.

Mhandisi wa Umwagiliaji mkoani Iringa Onesmo Kahogo amesema mwishoni mwa wiki mkoani Iringa kua, teknolojia hii inasaidia kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi, kwani itamsaidia mkulima kupima kiwango cha maji anayohitaji kutimia shambani na haina madhara kwa mazao.

Mhandisi Kahogo alisema Teknolojia hii imesaidia kupungua migogoro ya maji kwa wakulima na inampa mkulima nafasi ya kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.

Teknolojia hiyo inayotumia kifaa maalum kinachofukiwa nardhini ambacho, kinaruhusu eneo linalotumika kwa kilimo wa wakati huo kutumia maji yanayotosha kumwagiliwa katika eneo husika na kwa kiasi ambacho mkulima anakuwa amejipimia kulingana na mahitaji ya maji kwa wakati huo.

Kwa upande wake katibu wa skimu ya Kiwere maarufu kwa jina la tupendane Bw. Abdalah Taveli, amesema teknolojia hiyo inasaidia kupata mazao mengi kwa kutumia maji kidogo akitolea mfano ya mavuno ya gunia sabini za vitunguu katika hekari moja.

Alisema kuwa pamoja na teknolojia hiyo kutumia maji kidogo inasaidia pia matumizi madogo ya pembejeo, kutokana na kwamba hazisombwi na maji shambani. 
Mmoja wa wakulima wanaonufaika na Skimu ya Kilimo ya Umwagiliaji ya Kiwere wilayani Iringa inayotumia Teknolojia ya Kinyonga.
Mhandishi wa Umwagiliaji Mkoa wa Iringa, Onesmo Kahogo akizungumza kuhusu Teknolojia ya Kilimo cha Umwagiliaji maarufu kwa jina la Kinyonga.

No comments:

Powered by Blogger.