LIVE STREAM ADS

Header Ads

Trafiki matatani, TAKUKURU waweka mambo hadharani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Iringa imethibitisha kumkamata askari wa Usalama barabarani Copro Steven Mchomvu kwa tuhuma za kupokea rushwa eneo la Ipogolo Manispaa ya Iringa.


Na Fredy Mgunda, Iringa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Iringa imethibitisha kumkamata askari wa usalama barabarani kwa tuhuma za kupokea rushwa kwenye mabasi maeneo ya Ipogolo Manispaa ya Iringa tarehe 18/01/ 2022.

Kamanda TAKUKURU mkoani Iringa, Domina Mukama amemtaja askari huyo kuwa ni Copro Steven Mchomvu ambaye picha zake zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mukama amesema polisi huyo bado anashikiriwa na jeshi la polisi mkoani Iringa na taratibu zote zikikamilika atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

Amesema walimkuta na kiasi cha shilingi laki moja na nusu pesa taslimu ambazo alikuwa nazo mfukoni. Mukama ametoa onyo kwa watumishi wote wa Serikali kuacha tabia ya kutoa na kupokea rushwa kwa kuwa ni kinyume na Sheria za Utumishi wa Umma kulingana na kiapo cha kazi.

Aidha Mukama ameongeza kuwa wamefanikiwa kukagua jumla ya miradi kumi na mbili (12) yenye thamani ya shilingi bilioni saba milioni mia moja themanini, laki tano na elfu sabini na tisa na kumi na tano (7,135,579,015).

Amebainisha kuwa miradi hiyo ni ya sekta ya elimu, ujenzi (barabara) na afya ambayo ilikaguliwa kwa lengo la kujua thamani halisi ya pesa iliyotumika na na ubora wa miradi husika kama inaendana ambapo miradi yote ilikaguliwa na kukuta inaendelea vizuri na kwa ubora unaotakiwa.

Mukama amesema kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba mwaka 2021 walipokea jumla ya malalamiko 48 yanayohusiana na rushwa lakini baada ya uchunguzi waligundua kuwa taarifa za rushwa zilikuwa 26 na 22 hazihusiani na rushwa.

No comments:

Powered by Blogger.