LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Biteko apiga mkutano Kakola wilayani Kahama

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza na wananchi wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Kakola Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo alitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa shughuli za mgodi wa Bulyanhulu lazima ziwanufaishe wananchi.

Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko alisema Serikali imeendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wananchi ikiwemo madai ya fidia kutoka mgodi wa Bulyanhulu, kupata fursa za ajira katika mgodi huo pamoja na kuhakikisha fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zinatekeleza miradi yenye tija kwa wananchi.

Mkutano huo uliofanyika Jumanne Januari 25, 2022 Waziri Biteko aliwahimiza wanawake kuchangamkia fursa za uchumi wa madini kwa pia ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim na kulia ni Mkuu wa Mkoa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko alisema Serikali imeendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wananchi wa Msalala huku pia akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim (wa tatu kushoto) kwa namna anavyoshirikiana na wananchi katika shughuli za maendeleo pamoja na kutatua kero zilizokuwa zinahusiana na mgodi wa Bulyanhulu. 
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko.
Mkutani huo ulifanyika katika Kijiji cha Kakola, Msalala.
Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Dkt. Sophia Mjema (kulia) alimpongeza Waziri Biteko kwa kusimamia vyema sekta ya madini hususani kushughulikia changamoto za wananchi na mgodi wa Bulyanhulu.
Mbunge wa Jimbo la Msalala, Idd Kassim akizungumza kwenye mkutano huo ambapo alisema fedha za CSR zinazotolewa na mgodi wa Bulyanhulu zinazimamiwa vyema kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara.
Kamishna wa Tume ya Madini, Janeth Lekashingo akiwasabahi wananchi wa Msalala.
Kaimu Kamishna Wizara ya Madini, Maruvuko Msechu akiwasabahi wananchi baada ya kushiriki mkutano huo.
Mthamini wa Serikali kutoka Wizara ya Ardhi akiwasabahi wananchi.
Wananchi wakiwasilisha kero kwa Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko.
"Mhe Waziri tunaomba utusaidie kutatua kero zetu dhidi ya mgodi" 
Miongoni mwa kero za wananchi wa Kahama ni kupatiwa maeneo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini pamoja na kulipwa fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa na mgodi wa Bulyanhulu ambapo kuna waliolipwa na ambao bado kutokana na mvutano wa kisheria uliokuwepo.
Wananchi wa Msalala wakifuatilia mkutano huo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.