LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri wa Madini amtaka Mwekezaji Longido kufuata taratibu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoa wa Arusha, Dkt. Steven Kiruswa amemwagiza mmiliki wa mgodi wa PARAMOUNT LTD unaofanya shughuli za chimbaji katika Kijiji Cha Sinoniki na Kimwati katika Tarafa ya Engarenaibor wilayani Longido kuhakikisha anafuata taratibu za upataji wa eneo la ardhi kupitia kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji.

"Nimeona hapa Kimwati mmefuata utaratibu wote unaotakiwa,lakini Sinoniki hamjafuata taratibu naomba mkaliweke sawa kabla wizara haijachukua hatua Kali za kisheria lakini pia mkifuata taratibu mtaepuka migogoro na jamii" alisema Dkt. Kiruswa.

Dkt. Kiruswa aliwataka kufuata taratibu zote za kisheria ili kuepuka migogoro na jamii ikiwemo masuala ya uhifadhi wa mazingira pamoja na kuweka makubaliano yenye kuonekana kwa jamii ikiwemo kusaidia miradi ya Maendeleo.

"Nakuagiza Mwenyekiti wa Kijiji kaitisheni kikao Cha serikali ya Kijiji hata Cha dharau ,na ifikapo wiki ijayo taarifa ya makubaliano hayo yawe yamefika kwa Mkuu wa Wilaya Longido na sisi wizarani tutapata na kuangalia Kama yapo sawa" alisema Dkt. Kiruswa.
Hata hivyo aliwashauri wawekezaji hao kufanya utafiti zaidi(Exploration) kabla ya kuanza Uchimbaji au kuendelea kufanya Uchimbaji kwa kukisia pasipo kuwa na uhakika pomoja na kuweka utaratibu wa kusoma taarifa za miradi waliyoitekeleza kwa jamii katika mikutano mikuu ya vijiji.

Katika hatua nyingine aliwataka kutumia utaalamu wa kuchimba madini aina ya vito ili kuepuka uharibifu wa mazingira kwani maeneo hayo ni maeneo ambayo hutumika Kama korido ya wanyamapori na mifugo ya wananchi.

Dkt. Kiruswa aliwapongeza wawekezaji hao kwa kutoa fursa kwa vijana wazawa katika migodi hiyo,na kuwasisitiza kuwapa wanawake fursa za kuchakata mawe ili waweze kujiinua kiuchumi pamoja na kusisitiza ulinzi wa madini hayo pasipo kutorosha kupeleka nchini jirani kwani migodi hiyo ipo mpakani na Meto nchini Kenya.

No comments:

Powered by Blogger.