LIVE STREAM ADS

Header Ads

Majaliwa aweka msisitizo madini ya Tanzanite kuongezewa thamani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka watanzania kushirikiana na kushikamana ili kuyapa thamani madini ya Tanzanite na kuifanya dunia nzima itambue kuwa madini hayo yanapatikana Tanzania tu na tayari imeweka mazingira ya kuyaongezea thamani.

Mheshimiwa Majaliwa aliyasema hayo Jumatano Januari 26, 2022 alipozungumza na wananchi katika eneo la EPZA unapojengwa Mji wa Tanzanie katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Manyara.

Majaliwa alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha rasilimali zote zilizoko nchini yakiwemo madini ya Tanzanite zinawanufaisha wananchi wote hususani wanaoishi katika maeneo zinapopatikana. “Watanzania lazima tushirikiane na tushikamane kuyapa thamani madini hayo.”
Alisema kuwa Serikali itaendelea kukutana na wafanyabiashara wa sekta madini kwa lengo la kuhakikisha kwa pamoja wanaweka mikakati ya kusaidia kuikuza sekta hiyo ili iendelee kuleta tija kwa watanzania na taifa kwa ujumla.

Akizungumza baada ya kukagua eneo la uwekezaji la EPZA, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka watanzania kujitokeza na kuwekeza katika eneo hilo “Watanzania tumieni fursa ya eneo hili kuwekeza mtakapa faida”

Majaliwa aliwasisitiza wananchi waendelee kufanya biashara hiyo ambayo ina manufaa makubwa kwao na Taifa kwa ujumla na kwamba Serikali ipo tayari kuwahudumia wakati wote. “Tumejipanga kuwahudumia iwe wakati wa jua au wakati wa mvua.”
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.