LIVE STREAM ADS

Header Ads

Spika Ndugai aandamwa vibaya ‘mapya yaibuliwa’ jina liondolewe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa Mwanza umetoa tamko kali la kulaani baadhi ya viongozi ambao wameanza kutoa matamshi yanayolenga kukwamisha jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Tamko hilo limetolewa Januari 05, 2022 na Mwenyekiti wa umoja huo, Hellen Bogohe wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa wale wote wanaotoa matamshi hayo wanapaswa kulaaniwa vikali.
“Wanaosema nchi itauzwa kisa kukopa wanapaswa kulaaniwa kwani mama (Rais Samia) anakopa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na tunaona miradi mbalimbali inavyotekelezwa ikiwemo madarasa ya viwango kote nchini” ameonya Bogohe.

Tamko la UWT Mkoa Mwanza linakuja siku chache baada ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kunukuliwa akikosoa mpango wa Rais Samia kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo akisema nchi ikiendelea kukopa ipo siku itauzwa ambapo hata hivyo alijitokeza na kuomba radhi akisema alinukuliwa vibaya na mitandao ya kijamii.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.