LIVE STREAM ADS

Header Ads

Chanzo cha mauaji Tanzania chatajwa, Serikali yapewa mbinu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Viongozi wa Dini jijini Mwanza wakiongozwa na Kamati ya Amani wameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti matukio ya mauaji yanayoripotiwa katika mikoa mbalimbali nchini. Viongozi hao walitoa kauli hiyo Januari 31, 2022 wakati wa mkutano wa kutafuta suluhisho la kutokomeza mauaji hayo.

Wakati huo huo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani chini ya Waziri wake Mhandisi Hamad Masauni imeunda Kamati Maalum itakayokuja na mwarobaini wa kukomesha mauaji hayo ambapo Kamati hiyo imepewa siku 21 kukamilisha kazi hiyo huku Waziri Masauni akibainisha kuwa jeshi la polisi nchini linawashikilia watu 150 kwa kuhusishwa na mauaji katika mikoa mbalimbali.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.