LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyamagana ahitimisha semina kwa Madiwani jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi amehitimisha semina ya siku mbili iliyotolewa kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia maadili.

Makilagi amehitimisha semina hiyo Februari 11, 2022 na kuwahimiza washiriki kuyatumia vyema katika kutimiza majukumu yao huku kila mmoja akibadilika katika utendaji wake hususani kuepuka migongano ya kimasilahi.

Amesema semina hiyo iliyoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kutolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza ni muhimu kwa madiwani hao kwani itawasaidia kuwa viongozi bora watakaoepuka mgongano wa kimaslahi kazini na hivyo kuwahimiza kuyazingatia.

"Ukiwa na maadili utakuwa na nidhamu ya kazi, kiongozi bora, kiongozi wa mfano na hutajuta, mimi sijisemi lakini sijawahi kujuta na najipambanua hivyo" amedokeza Makilagi akiwahimiza madiwani hao kubadilika na kuzingatia maadili katika utendaji wao wa kazi.

Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Rodrick Ngoye amesema watafanyia kazi yale yote waliyojifunza na kwamba Halmashauri hiyo itaendelea kuwajengea uwezo madiwani wake kupitia mafunzo mbalimbali ili kutimiza vyema majukumu yao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Nyamagana Amina Makilagi (kushoto) akihitimisha semina kwa madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Katikati ni Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Rodrick Ngoye na kulia ni Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza, Godson Kweka.
Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza Rodrick Ngoye.
Mwanasheria kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza, Abigael Majige akiwasilisha mada kwenye semina hiyo.
Madiwani wakifuatilia semina hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.