LIVE STREAM ADS

Header Ads

TCRA yafafanua bei za Data kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Ufafanuzi huo umetolewa leo Mei 9, 2022 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari akizungumza na waandishi wa habari.

Dkt. Bakari ameanza kwa kueleza kuwa bei za huduma za mawasiliano ya simu zimegawanyika katika makundi mawili, ambayo ni bei za kawaida na bei za huduma ndani ya vifurushi.

“Bei za kawaida (nje ya vufurushi) ni bei wanazolipa watumiaji wa huduma za kupiga simu, kutumba jumbe fupi au matumizi ya data bila ya kujiunga na vifurushi” amesema Dkt. Bakari.

Aidha amesema, huduma za vifurushi zinaambatana na masharti ya kikomo cha muda pamoja na matumizi ambayo ametolea mfano kuwa ni vifurushi vya siku, wiki, mwezi, vya wanachuo, vya siku, vya maneno maalum na kadhalika ambavyo huwa vinabadilika kutokana na uhitaji.

“Kwa lugha nyepesi, vifurushi ni sawa na “buffet” ambapo mteja anaweza kula au kunywa chochote kilichopo kwenye “package” hiyo ndani ya muda maalum” amefafanua Dkt. Bakari.

Amebainisha kwamba vigezo mbalimbali vinavyotumika na watoa huduma katika kupanga bei za huduma za mawasiliano ikiwemo data ni pamoja na gharama za uwekezaji na uendeshaji, idadi ya watoa huduma na muundo wa soko, Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta, ukubwa wan chi na upatikanaji wa rasilimali wezeshi za mawasiliano.

Dkt. Bakari ameeleza kwaba takwimu zinaonesha kuwa zadi ya asilimia 95 ya watumiaji wa huduma za mawasiliano wanapendelea kutumia huduma za vifurushi kwa kuwa zina punguzo kubwa, hivyo kuweka unafuu katika matumizi ya huduma za mawasiliano.

“Endapo mtumiaji ataamua kutumia data bila kujiunga kufurushi atatozwa bei za kawaida” amesema.

Aidha ameeleza, suala la data kuisha haraka huchangia na sababu mbalimbali zikiwemo kuongezeka kwa kasi ya mtandao na uwezo wa Simu-Janja, kuongezeka kwa ubora wa picha na video zinazojihuisha mara kwa mara bila mtumiaji kujua.

“TCRA ina utaratibu wa kufanya stadi za bei za huduma za mawasiliano ambapo stadi ya sasa inaonesha kuwa, gharama halisi ya kuuza data hapa nchini ni kati ya TZS 2.03/Mb hadi TZS 9.35/Mb. TZS 2.03/Mb ni bei ambayo mtoa huduma anaweza kuuza Data na kurudisha gharama zake za uendeshaji na TZS 9.35/Mb ni bei ambayo mtoa huduma anaweza kuuza data na kutoa huduma zenye ubora na kuwafikia wananchi wengi zaidi” amesema Dkt. Bakari.

Amesema kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za bei za huduma za data, Tanzania kwa sasa ndiyo ina bei ya chini zaidi kwa Mb kwa nchi za Afrika Mashariki na SADC ambapo wastani wa gharama za data nchini ni takribani dola 0.75 za Kimarekani kwa Gb moja ya data sawa na shilingi za kitanzania TZS 1,725 (sawa na TZS 1.68/Mb).

Aidha amebainisha kuwa kwa barani Afrika, Tanzania ni miongoni mwa nchi sita kati ya 52 zenye gharama nafuu za data.

Ameeleza kwamba, Kanuni ya Mawasiliano ya Kielekroniki na Posta (bei za huduma) ya mwaka 2018 inamtaka mtoa huduma kuwasilisha bei zake kwa TCRA kila robo mwaka.

“Bei zilizowasilishwa, kuidhinishwa na ambazo zinatumika hivi sasa ziko ndani ya wigo wa bei uliokubalika. Bei ya data kwa sasa inaanzia TZS 1.5/Mb hadi TZS 9.35/Mb” ameeleza Dkt. Bakari.
Watendaji wa TCRA na waandishi wa habari wakifatilia mada wakati mkutano wa waandishi habari kuhusiana na Data.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk.Jabiri Bakari akizungumza na waandishi wa habari kihusiana na hali ya gharama za Data kwa watumiaji wa mawasiliano, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk.Emmanuel Manase akitoa mada namna ya gharama za data zinavyokwenda nchini jijini Dar es Salaam.

No comments:

Powered by Blogger.