LIVE STREAM ADS

Header Ads

Antonia kuzindua Albamu yake mjini Morogoro

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka Morogoro, Antonia Emmanuel.
***

Na Fabian Fanuel, Morogoro
Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka mjini Morogoro, Antonia Emmanuel amewahakikishia watu wote watakaohudhuria uzinduzi wa albamu yake iitwayo Nasikia Maneno Maneno watabarikiwa sana.

Akizungumza na Famara Media, Antonia amesema kila kitu kinaenda vizuri katika maandalizi, na anachokifanya kwa sasa ni kuzidi kumalizia hatua zote ili afanye uzinduzi wa kihistoria mjini Morogoro katika kanisa la TGRC Mazimbu Barakuda.

"Maandalizi ya uzinduzi yanazidi kukamilika, kila idara husika inafanya kazi ili kuhakiki tamasha hili la Uzinduzi linafana sana na kuweka historia mpya katika tasnia ya muziki wa Injili Tanzania" alisema Antonia Emmanuel.

Antonia amesema ana faraja maana watu mbalimbali walioalikwa wameonyesha mwitikio mkubwa wa kushiriki. Amewataja waimbaji na wageni waalikwa wamekuwa wakimpigia simu ili kujua maandalizi yanakwendaje, hii ikiwa ishara nzuri kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo.

Emmanuel amesema amekuwa anapata sapoti kubwa kutoka kwa Mchungaji wake Jailos Maloda na wakristo wanaoabudu kanisani hapo, hii ikiwa ni ishara ya mshikamano na umoja uliopo kati yao washirika waosali katika la TGRC Mazimbu Barakuda Morogoro.

Aidha amesema ameomba waombaji popote walipo nchini Tanzania na nje ya nchi kuendelea kumwombea na kuombea uzinduzi wake ili ufanikiwe zaidi kama anavyokusudia moyoni mwake.

Albamu ya Antonia Emmanuel ina jumla ya nyimbo nane ambayo itazinduliwa tarehe Julai 24, 2022 katika Kanisa la TRGC linalochungwa na Mchungaji Jailos Maloda.

No comments:

Powered by Blogger.