LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watumishi wa Wizara ya Madini wapigwa msasa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wizara ya Madini inaendelea na mafunzo ya ununuzi na ugavi kwa Idara na Vitengo vya Wizara ya Madini.

Mafunzo hayo yametolewa kwa Idara na Vitengo mbalimbali Juni 21, 2022. Mfunzo hayo yanatolewa kwa Kitengo cha Mawasiliano Serikalinj (GCU) na Kitengo cha TEHAMA (ICT) katika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma.

Katika mafunzo hayo, watumishi wanapatiwa mafunzo ya taratibu za ununuzi kuanzia kwa mtumiaji hadi katika Kitengo cha Menejimenti ya Usimamizi wa Ununuzi (PMU) kwa mujibu wa Sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016.

Pia yatatolewa mafunzo kuhusu mpango wa manunuzi ya Wizara ya Madini unaotokana na bajeti ya kila mwaka. Aidha mafunzo kuhusu utaratibu wa utoaji mafuta na mifumo ya mafuta ya GPSA na mfumo wa wizara.
Picha na Wizara ya Madini

No comments:

Powered by Blogger.