LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mfuko wa WCF watoa Semina kwa waajiri jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetoa semina ya siku moja kwa waajiri mkoani Mwanza, kwa lengo la kutoa elimu ya kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa taarifa za polisi katika ulipaji wa fidia.

Semina hiyo imefanyika Jumanne Juni 21, 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Fedha (IFM) kampasi ya Mwanza uliopo kwenye jengo la Rock City Mall jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter amesema mfuko huo umekuwa ukikutana na changamoto katika kutoa huduma hasa kwenye upande wa kulipa fidia kwa wafanyakazi kutokana na kukosekana kwa taarifa za polisi zinazothibitisha kutokea kwa ajali hali inayopekekea mtumishi kutolipwa fidia kwa wakati.

Amesema kutokana na changamoto hiyo, uongozi wa WCF umeamua kutoa elimu kwa waajiri ili na wao wakawaelimishe wafanyakazi wao kuhusu umuhimu wa kuwasilisha kwa wakati taarifa za kipolisi pindi mfanyakazi anapopata madhira kazini ili alipwe fidia.

"Katika kutekeleza jukumu letu la kulipa fidia kwa wafanyakazi, mfuko una kazi kubwa ya kujenga mifumo ya kutuwezesha kutoa huduma, lakini tunaaamini mifumo pekee yake haiwezi na ndio maana tunawafanyakazi wenye weledi kwa ajili ya kutoa huduma hivyo tuna imani mkiwezeshwa itarahisisha taasisi kutoa huduma bora pamoja na waajiri kuzifikia huduma zetu kwa urahisi" amesema Peter

Amesema semina hiyo itawajengea uelewa wa namna ya kupata huduma WCF pamoja na mafao yanayotolewa na mfuko huo.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Wilbroad Mutafungwa amesema wao wanahusika moja kwa moja katika upelelezi, uchunguzi wa taarifa zote za wafanyakazi ambazo zimeripotiwa kwenye vituo mbalimbali vya polisi na kuzichunguza na kuwasilisha ripoti inayosaidia mfanyakazi aliyeumia kazini kulipwa fidia na WCF.

"Tunawahimiza sana waajiri kuweka kumbukumbu nzuri za wafanyakazi pamoja na kuhakikisha mnawasaidia kutoa taarifa pale wanapokumbwa namatukio ya ajali" amesisitiza Mutafungwa

Amesema waajiri walioshiriki semina hiyo wamepata elimu itakayowasaidia kubadilisha mtizamo wa wafanyakazi hususani kutambua kwamba hata kama tatizo ni dogo lazima lilipotiwe polisi ili waweze kupata haki zao kwa wakati.

Naye Lawrence Ndagula ambaye ni mmoja wa washiriki wa semina hiyo kutoka kampuni ya Mwanza Huduma amesema elimu waliyoipata itawasaidia kujua umuhimu wa kupeleka taarifa polisi pindi mfanyakazi anapopata ajali akiwa kazini.

Kwa upande wake Afisa Rasirimaliwatu kutoka kampuni ya Fluiconnecto, Azza Azzuna amesema semina hiyo imemwongezea wigo mpana wa kuwasaidia wafanyakazi wake kupata stahiki zao pindi wanaumia wakiwa kazini.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Anselim Peter akifungua mafunzo ya siku moja kwa waajiri mkoani Mwanza yenye lengo la kuwajengea uwezo hususani umuhimu wa kutuma kwa wakati taarifa za wafanyakazi wao pindi wanapopata madhira kazini ili kulipwa fidia.
 Kamada wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Wilbroad Mutafungwa (kulia) akizungumza kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo waajiri mkoani Mwanza yaliyoandaliwa na Mfuko wa WCF. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi wa kutoka kampuni ya Barrick, Daniel John akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Waajiri kutoka taasisi na makampuni mbalimbali jijini Mwanza wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya waajiri jijini Mwanza wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na mfuko wa WCF ili kuwawezesha kutambua umuhimu wa kutuma taarifa sahihi na kwa wakati pindi mfanyakazi anapopata madhira kazini.
Baadhi wa waajiri jijini Mwanza wakifuatilia semina hiyo.
Picha na Michael Jamson, Mwanza

1 comment:

  1. Others will offer adjustable coin values enable you to|which let you} guess a lot as} tons of or 1000's per spin. Playing high stakes slots supplies the potential to win big 파라오카지노 도메인 payouts. High variance slots involve a better degree of threat, but they provide the potential for larger rewards. When you play such slots, you will land winning combinations occasionally. You may see your bankroll reduce considerably earlier than you hit a good sized win, so they are greatest for knowledgeable players with an enormous price range and time to spare. Medium variance slots are a good compromise between slots with low and high variance.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.