LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau walaani mauaji ya watoto mkoani Geita, wataka hatua zichukuliwe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa OJADACT, Edwin Soko (kushoto) akizungumza na wanahabari jijini Mwanza.
***

Chama cha Waandishi wa Habari wanaopinga matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT) kinalaani matukio ya mauaji yanayoendelea nchini husasani matukio mawili ya mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Geita.

Tukio la kwanza lilihusisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la saba Johson Thomas (14) katika Shule ya Msingi Buhalahala Halmashauri ya Mji Geita aliyekutwa amefariki na mwili wake ukiwa pembeni mwa Mto baada ya kupotea Juni 02, 2022.

Tukio la pili ni tukio la kuuawa kwa mtoto Dorcas Mathias (07) aliyekuwa Mwanafunzi wa Chekechea Shule ya Msingi Ibambi wilayani Nyahg’wale baada ya kuvamiwa na watu watatu wakati akiwa anachunga mbuzi na mwenzake.

Itakumbukwa Kamanda wa Polisi mkoani, Geita Henry Mwaibambe alisema baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi na Daktari ilibainika kuwa mtoto huyo alibakwa, kulawitiwa na kisha kuuawa na baadaye akavunjwa shingo. Jeshi la Polisi limewafikisha mahakamani watuhumiwa watatu kwa kuhusishwa na tukio hilo.

Watuhumiwa hao ni Mathias Shilole (26) mkulima, Sita Makabila (52) mganga wa tiba asili na Lucy Mdelema wote wakazi wa Geita.

OJADACT imebaini sababu mbalimbali za maujai hayo ni pamoja na
01. Imani za kishirikina kwenye jamii zinahusishwa na kujipatia utajiri kwa njia nyepesi
02. Ukatili kwenye jamii unaombatana na malezi mabaya ya jamii isiyo na staha

OJADACT inatoa rai kwa jamii kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa Sheria na badala yake jamii iwe mlinzi wa mtoto kwa kutoa tarifa inapoona viashiria vya ukiukwaji wa haki za mtoto ikiwemo haki ya kuishi.
Serikali na wadau mbalimbali waendelee kufanya kazi kwa pamoja ILI kuwalinda watoto.
Edwin Soko
Mwenyekiti
OJADACT
22.06.2022

No comments:

Powered by Blogger.