LIVE STREAM ADS

Header Ads

NBS yawanoa Waandishi wa Mitandaoni kuhusu Sensa ya Watu na Makazi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari na wahariri zaidi ya 50 kutoka vyombo vya habari vya mitandaoni (Blogs & Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini kuhusu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza Jumanne Juni 14, 2022 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa ambapo NBS inaendelea kutoa mafunzo ya aina hiyo pia kwa wadau mbalimbali watakaosaidia kufanikisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kufanyika Agosti 23, 2022.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo, Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka NBS, Said Ameir amesema waandishi wa habar/ vyombo vya habari ni miongoni mwa wadau muhimu katika kuhamasisha jamii kushiriki zoezi la Sensa.

Amesema maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mwaka huu 2022 yako vizuri na kwamba matarajio ni kukamilika mapema na kwa wakati kutokana na matumizi ya teknolojia ya kisasa inayotumika kukusanyia takwimu ambapo maswali yote muhimu yatakuwa pia kwenye vishikwambi na hivyo kuwarahisishia makarani kujaza taarifa kidigitali.

Amesema zoezi la Sensa nchini hufanyika kila baada ya miaka 10 na lina manufaa makubwa kwa jamii kwani husaidia Serikali kupata taarifa na takwimu muhimu kwa ajili ya mipango ya maendeleo na hivyo kuwahimiza wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wakati wa zoezi hilo.

Kwa upande wake Mratibu wa Jukwaa la Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) ambaye pia ni Mkurugenzi Gilly Bonny TV amesema mafunzo hayo ni muhimu na yatawasaidia waandishi wa habari wa mitandaoni kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ili makarani watakapokuwa wanapita kwenye kaya zao wawape ushirikiano na wasiwe na hofu ya kujibu maswali watakayoulizwa.

Washiriki wa mafunzo hayo watajengewa uelewa kuhusu mada mbalimbali ikiwemo Sensa na Sheria ya Takwimu, umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi na maandalizi yake, madodoso ya Sensa maudhui yake, teknolojia katika Sensa ya watu na makazi kutoka kwenye makaratasi hadi kwenye vishikwambi.

Pia watakumbushwa wajibu wa vyombo vya habari katika kufanikisha Sensa ya watu na makazi 2022, vyanzo vikuu vya uripoti kwenye Sensa ya watu na makazi, maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu Sensa pamoja na mbinu za kuripoti habari za Sensa.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG 
Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka NBS, Said Ameir akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mwanasheria NBS, Mary Senapee akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo ambapo amesema kwa mjibu wa Sheria, Karani wa Sensa ya Watu na Makazi kutoa ama kutumia taarifa kwa maslahi yake binafsi hivyo wananchi wasiwe na hofu kwani taarifa watakazotoa zitakuwa ni siri na zitatumika kwa mipango ya maendeleo tu.
Mtaalamu wa Idadi ya Watu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Hellen Siriwa amesema Sensa ya mwaka huu 2022 itakuwa ya sita ambapo Sensa ya kwanza ilifanyika mwaka 1967 ikiwa na watu milioni 12.3, Sensa ya pili ya mwaka 1978 watu milioni 17.5, Sensa ya tatu ya mwaka 1988 watu milioni 23.1, Sensa ya nne ya mwaka 2002 watu milioni 34.4 na Sensa ya mwaka 2022 matarajio ni watu milioni 61.3 ambapo itakuwa Sensa ya kwanza kutumia mfumo wa kidigitali.
Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu NBS, Bededict Mugambi akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu NBS, Bededict Mugambi (kushoto) akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya mtandaoni (kulia) kuhusu maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi 2022.
Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 yanayofanyika mjini Iringa ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Jukwaa la Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA).
Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi 2022.
Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka NBS, Said Ameir akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa Habari wakifuatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Mitandao ya Kijamii wakifuatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa Habari wa Mtandaoni wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mtandaoni wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi.

Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mtandaoni wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi 2022.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mtandaoni wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mtandaoni wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi.
Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii wakiwa kwenye mafunzo kuhusu Sensa ya Watu na Makazi yaliyoratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Kwa kushirikiana na Jumuiya Mitandaoni ya kijamii Tanzania (JUMIKITA)

No comments:

Powered by Blogger.