LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makundi 19 Nyamagana yapewa elimu ya Sensa “wataelimisha wenzao”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kamati ya Sensa ngazi ya Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, imetoa elimu kwa makundi mbalimbali ya kijamii wilayani humo ili kutambua umuhimu wa kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amesema wawakilishi wa makundi ya kijamii walipata elimu hiyo watakuwa mabalozi kwa wenzao na kwenda kuwaelimisha ili kufahamu manufaa ya Sensa na kushiriki ipasavyo.

Alisema Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi muhimu kwa Taifa kwani inasaidia Serikali kupata taarifa muhimu zitakazosaidia kupata mipango ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali na hivyo kuwahimiza wananchi kutoa ushirikiano wakati wa zoezi hilo.

Makilagi aliwatoa hofu wananchi kwamba taarifa zote muhimu watakazozitoa zitakuwa za siri za zitatumika kwa masuala ya kimaendeleo tu hivyo wakuu wa kaya wanapaswa kuwapa ushirikiano makarani wa Sensa watakapokuwa wanapita katika kaya zao kufanya mahojiano nao.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima alitoa rai kwa madiwani wa halmashauri hiyo kupitia Kamati za maendeleo ya Kata kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili zoezi hilo lifanikiwe na kuleta tija kwa taifa.

Sima aliwatoa hofu wananchi hususani vijana watakaokuwa wamelala kwenye nyumba za kulala wageni usiku wa kuamkia zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwamba wasiogope kutoa taarifa zao kwani zitakuwa za siri.

Kwa upande wake Mratibu wa Sensa Wilaya ya Nyamagana, Costantine Ruhinda alisema makundi 19 yameshiriki kongamano hilo ikiwa ni pamoja na NGO’s, bodaboda, madereva daladala, bajaji, wafanyabiashara wadogo, waalimu, wanasiasa, waandishi wa habari, vijana, akina mama, wenye ulemavu, taasisi binafsi na za Serikali ili wakahamasishe wenzao kwani Sensa ya Watu na Makazi kwani inahitaji hamasa ya wananchi ili kufanikiwa.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo akiwemo Mwl. Teddy Nyenza waliahidi kufikisha elimu waliyoipata; “nitakwenda kufundisha wanafunzi nikiamini kwamba wao pia watafikisha elimu hiyo kwa ndugu zao”.

Kongamano hilo lilifanyika Jumamosi Juni 11, 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Butimba jijini Mwanza likiwa na ujumbe usemao "Sensa kwa Maendeleo, Wilaya ya Nyamagana Tujiandae Kuhesabiwa".
Na George Binagi-GB Pazo, BMG
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la elimu ya Sensa wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la elimu ya Sensa wilayani humo.
Washiriki wakifuatilia ufunguzi wa kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (katikati) akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la elimu ya Sensa wilayani humo. Kulia ni Mratibu wa Sensa Wilaya ya Nyamagana Costantine Ruhinda na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Selemani Sekiete.
Mratibu wa Sensa Wilaya ya Nyamagana, Costantine Ruhinda akizungumza kwenye kongamano hilo.
Wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa mashirika binafsi wakifuatilia kongamano hilo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo.
Wadau wakifuatilia kongamano hilo.

No comments:

Powered by Blogger.