LIVE STREAM ADS

Header Ads

OJADACT yahimiza matumizi ya Takwimu kwa Waandishi wa Habari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waandishi wa Habari wametakiwa kutumia takwimu katika uandaaji wa habari na makala mbalimbali ikiwemo zinazohusiana na uendelevu wa fukwe za Bahari na maziwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko ametoa rai hiyo Juni 11, 2022 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uwazi wa takwimu.

Soko amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuisaidia jamii kutambua umuhimu wa katunza mazingira majini na nchi kavu ili kusaidia uendelevu wa fukwe nchini kwa manufaa mbalimbali hususani ya kiuchumi.

Amesema takribani asilimia 57 ya uchumi wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, unategemea shughuli za maziwa na bahari hivyo jamii kutowajibika kwenye utunzaji wa mazingira inaweza kusababisha joto kali duniani na matokeo yake ni fukwe kupotea na kudhorotesha manufaa yake.

Naye Mratibu OJADACT, Lucy Kilanga amesema kumekuwa na changamoto ya matumizi ya takwimu kwenye Habari zinazohusu ustahimilifu/ uhimilivu wa fukwe za bahari na maziwa na hivyo kuwasihi waandishi wa habari kufanyia kazi changamoto hiyo kwa kutumia takwimu zinazotolewa na mamlaka mbalimbali.

Nao baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Innocent Alloyce na Beatrice Rabach wameomba taasisi za umma na binafsi zinazojihusisha na uhifadhi wa mazingira kuwajengea uwezo ili kuwasaidia kufuatilia masuala ya uhifadhi wa rasilimali Bahari na maziwa.

Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na OJADACT kwa kushirikiana na Shirika la Open Knowledge Foundation yakiwa na kaulimbiu isemayo 'Uwazi wa Takwimu kwenye Kuimarisha maisha ya Wote' yamewashirikisha waandishi wa habari zaidi ya 25 kutoka mkoani Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa OJADACT, Edwin Soko (kulia) akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mratibu OJADACT, Lucy Kilanga (kulia) akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mwanahabari Glory Kiwia (kulia) akichangia hoja kwenye maadhimisho hayo.
Waandishi wa Habari jijini Mwanza.
Shughuli zinazofanyika fukweni ziendane na utunzaji wa mazingira ili kuendeleza uhimilivu wa fukwe hizo.
Picha ya pamoja.
Wasaa wa viburudisho.

No comments:

Powered by Blogger.