LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi wa Umma watakiwa kufanya kazi kwa Uadilifu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kamishina wa Tume ya Maadili, Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi akizungumza na watumishi wa Mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma wakati Tume hiyo ilipokwenda kuzungumza kuhusiana na Maadili.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Gabriel Robart akizungumza wakati akimkaribisha Kamishina wa Tume ya Maadili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo katika wiki ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Kamishina wa Tume ya Maadili hayupo pichani wakati maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo Tume ya Maadili imekwenda kuwanoa kuhusiana na maadili.
Kamishina wa Tume ya Maadili Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza.
***

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Kamishna wa Tume ya Maadili Jaji wa Rufani Tanzania, Sivangilwa Mwangesi amewataka Viongozi wa Umma kufanya kazi kwa Uadilifu na kutojiingiza katika vitendo vinavyopelekea ukiukwaji wa Maadili.

Mwangesi aliyasema hayo katika kikao chake na Viongozi wa Mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16 hadi Juni 23 ambapo Ofisi Tume ya Maadili imefanya kikao na watumishi wa Mkoa wa Mwanza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mwangesi aliwaasa Viongozi hao kitojiingiza katika mgongano wa Maslahi jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Aliongeza kuwa endapo viongozi watawajibika katika maeneo yao ya kazi kwa uadilifu itapelekea kujenga imani kwa wananchi wanaowaongoza na Serikali kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi alifafanua kuwa Maadili ni hatua muhimu inayo tambulisha mtu ndani ya Jamie husika na maadili hujitokeza katika matendo yake.

Mhandisi Robert aliongeza kuwa lengo la kikao hiki ni kuunga mkono jitiihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kupinga vitendo vya Rushwa, Ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za Umma.

Maadhimisho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini yalianza rasmi Juni 16 na yatahitimishwa Juni 23, 2022

No comments:

Powered by Blogger.