LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA: Shule ya Sekondari Ibinza yafanikiwa kupambana na Ziro

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Mwl. Marco Busungu (kushoto) akimkabidhi cheti cha pongezi Mkuu wa Shule ya Sekondari Ibinza, Mwl. Igweselo Kahagi (kulia) baada ya Shule hiyo kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka jana 2021.
***

Shule ya Sekondari Ibinza iliyopo Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza imefanikiwa kupambana na matokeo hafifu ya daraja ziro kutoka wanafunzi 51 mwaka 2015 hadi kufikia wanafunzi sita mwaka 2021 ambapo matarajio ni kuondoa ziro katika mitihani ijayo ya kitaifa.

Mafanikio hayo yametokana na jitihada za uongozi wa shule hiyo kwa kushirikiana na wazazi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ikiwemo Shirika la Kutetea Haki za Watoto na Wanawake KIVULINI lenye makao yake makuu katika Kata ya Nyamhongolo ilipo Shule hiyo ya Ibinza Sekondari.

Katika kutoa hamasa zaidi kwa waalimu na wanafunzi  wa Shule hiyo ili kufikia lengo la kuondoa ziro kwenye matokeo ya kidato cha pili na nne mwaka huu 2022, shirika la KIVULINI limefanikisha sherehe ya pongezi kwa waalimu na wanafunzi wa Shule hiyo ya Ibinza Sekondari baada ya kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana 2021.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ibinza, Mwl. Igweselo Kahagi akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi na waalimu wa Shule hiyo kutokana na matokeo mazuri ya kidato cha nne mwaka 2021.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye hafla hiyo.
Afisa Miradi Mwandamizi Shirika la KIVULINI, Grace Mussa alisema shirika hilo limesaidia kutoa elimu kwa wanafunzi ili kujitambua na kujiepusha na vishawishi kwa lengo la kutimiza malengo yao kielimu.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Mwl. Marco Busungu akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ibinza (kulia) akipongezwa baada ya kufanya vizuri kwenye masomo yake.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ibinza wakiwa kwenye hafla hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.