LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Biteko awatoa hofu wachimbaji madini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amesema maeneo yenye madini katika hifadhi bado yanatafutiwa ufumbuzi ili wachimbaji waweze kuchimba na kunufaika na rasilimali hiyo.

Dkt. Biteko alisema hayo Julai 01, 2022 alipotembelea na kuzungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Lugelele wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya katika ziara yenye lengo ya kukagua shughuli za uchimbaji madini na kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji hao wa madini ya dhahabu.

Aliongeza kuwa Serikali inayatafutia ufumbuzi maeneo yaliyopo kwenye hifadhi ili kuwawezesha wachimbaji na hivyo kunufaika na rasilimali madini.

Alifafanua kuwa maeneo yaliyopo chini ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) bado hayaruhisiwi kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo mpaka sasa. Aidha kwenye hifadhi za misitu amefafanuwa kuwa, Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) haijazuia shughuli za uchimbaji madini.

"Maeneo ya hifadhi ya wanyamapori hakuruhusiwi shughuli za kibinadamu, za uchimbaji madini zinazoruhusiwa ni za aina mbili tu, kutafiti mafuta na gesi na kuchimba madini ya nishati" alisisitiza Dkt.Biteko.
Aliongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anataka kuwaona wachimbaji wanapewa fursa kwenye uchimbaji wa madini ili waweze kunufaika na rasilimali madini.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune alisema kuwa, shughuli za uchimbaji madini katika wilaya hiyo zimekuwa fursa kwa wananchi katika kujipatia kipato cha kila siku.

Alisema wachimbaji wengi wanapata ajira katika maeneo hayo na amemweleza Waziri Biteko kuwa, wilaya ya Mbarali inapata wastani wa kilo 2.5 ya dhahabu ambayo huchangia kwenye Pato la Taifa na halmashauri hiyo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko alitembelea kiwanda cha kuzalisha kokoto cha TAZARA Kongolo Quarry ili kujionea shughuli zinazofanyika katika kiwanda hicho.
Na Steve Nyamiti, WM

No comments:

Powered by Blogger.