LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yahamasisha matumizi ya gesi kwa kugawa mitungi bure

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali kupitiwa Wizara ya Nishati imeanza kutekeleza mpango wa kugawa mitungi ya gesi bure kwa makundi maalumu kama mamalishe na walimu ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa hatua itakayosaidia kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa umeme.

Waziri wa Nishati, January Makamba ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza na kuongeza kuwa Wizara imetenga zaidi ya Bilioni 10 kutekeleza mpango huo.

Waziri Makamba pia amekabidhi mitungi yenye gesi kwa mamalishe walio eneo Busisi wilayani Sengerema. Pia waalimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe watanufaika na mpango huo.

Hatua hiyo ni sehemu ya utafiti wa matumizi ya Nishati safi na salama yanavyoweza kusaidia utunzaji wa mazingira na kuzuia ucharibufu wa vyanzo vya maji ambapo mitungi ya gesi ipatayo 5,000 itatolewa kwa wananchi ambao baadae wataeleza unafuu wa matumizi ya gesi kulinganisha na kuni ama mkaa.
Tazama BMG TV hapa chini
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

No comments:

Powered by Blogger.