LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uongozi usitufanye tuache kumtumikia Mungu- DC Kongwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Remidius Mwema ameitaka jamii hususani vijana wanaopata nafasi za kuwa viongozi wa nyadhifa mbalimbali kujitoa kikamilifu katika kusaidia kazi ya Mungu kwani maisha na utumishi wao vitapimwa ni kiasi gani wamegusa maisha ya watu wengine.

Mwema ametoa nasaha hizo kwenye uzinduzi wa albamu ya kwaya ya kwaya ya Mizeituni iliyoambatana na harambee katika kanisa la EAGT Kongwa linaloongozwa na Askofu Dkt, Dennis Livingstone.

"Nimefurahi kuona kundi kubwa la vijana wakimtumikia Mungu, na sisi ambao Mungu ametupa neema ya kuteuliwa katika nyadhifa hizi za kuwatumikia watu na hasa vijana ni lazima tujifunze kuendelea kumtumikia Mungu" alisema Mwema na kuongeza;

"Tunachojifunza ni kwamba tunapokuwa viongozi na kupata nyadhifa mbalimbali hiyo sio tiketi ya kutofanya kazi ya Mungu, hivyo nitoe rai kwa vijana wenzangu, tujitahidi sana kumtumikia Mungu na tumuombe atupe hekima na busara katika kazi tunazozifanya" aliongeza Mwema.
Pia aliipongeza kwaya hiyo kwa huduma yao ya uimbaji kwani ni njia moja wapo ya kulifikisha mbele neno la Mungu, wakitimiza agizo lisemalo enendeni ulimwenguni kote mkahubiri injili.

Mwema alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waumini wa kanisa hilo kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambalo litafanyika nchi nzima Agosti 23, 2022.
Kwa upande wake kiongozi wa kanisa hilo Askofu, Dkt Living Stone Dennis alimshukuru mgeni rasmi kwa kukubali mwaliko wao huku akiitaja kwaya hiyo kuwa ndio kwaya ya kwanza kanisani hapo ambayo ilianzishwa miaka 1982.

Katika risala yao, waimbaji wa kwaya hiyo waliomba mgeni rasmi awasaidie kuchangisha kiasi cha fedha zaidi ya milioni 13 ambazo zitatumika katika ununuzi wa kiwanja cha ujenzi wa nyumba za kupangisha ambazo zitakuwa mradi wa kwaya.
Kwaya ya Mizeituni iliyopo Kanisa la EAGT Kongwa.
Na Maganga Gwensaga, Dodoma

No comments:

Powered by Blogger.