LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza afungua Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima amefungua rasmi Maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi Kanda ya Ziwa Magharibu yanayofanyika katika uwanja wa Nyamhongolo.

Akifungua Maonesho hayo Agosti 05, 2022, Malima ameziagiza Halmashauri mkoani Mwanza kuweka mikakati ya kuhimiza kilimo cha umwagiliaji hatua itakayosaidia wakulima kupata mavuno yenye tija na kukabiliana na uhaba wa chakula unaotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema Mkoa Mwanza unakadiriwa kuwa na ardhi kiasi cha hekta 36,000 kwa ajili ya kilimo cha unwagiliaji lakini ni hekta 1635 sawa na asilimia 4.5 zimetumika na hivyo kutoa rai kwa wakulima kuchangamkia fursa hiyo.

Aidha amesisitiza wakulima kufuata Kanuni za kilimo bora wanapoandaa mazao ya chakula na biashara hatua itakayosaidia kuongeza uzalishaji ikizingatiwa huku uwepo wa Ziwa Victoria ukiongeza fursa zaidi katika kilimo cha unwagiliaji.

Taasisi, mashirika, Halmashauri na wadau mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kutoka mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera kutangaza bidhaa mbalimbali za kilimo, mifugo na uvuvi huku wengine wakitoa elimu kwa wananchi kupitia Maonesho hayo ya Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi.
Maonesho hayo yamechagizwa na kaulimbiu isemayo "Ajenda 10/30, Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi" ikihamasusha wananchi kujiandaa kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23, 2022 lakini pia kukuza mchango wa sekta ya kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
Na BMG Habari 

No comments:

Powered by Blogger.